Jumapili, 17 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Enyi Waislamu: Maisha Yenu Yanawezaje Kuwa Mazuri Wakati Wanawake Walio Huru Wako Katika Magereza ya Mayahudi, Wakiteswa na Heshima Zao Zikivunjwa?!

Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Palestina kilifichua, kulingana na ushuhuda mpya uliokusanywa na mawakili na watafiti wa kituo hicho kutoka kwa wafungwa kadhaa walioachiliwa huru kutoka Ukanda wa Gaza kutoka magereza na vituo vya uzuizi vya umbile la Kiyahudi, utaratibu na mpangilio wa mateso ya kingono, ikiwemo ubakaji, kuvua nguo, kulazimishwa kurekodi filamu, na unyanyasaji wa kingono kwa kutumia zana na mbwa, pamoja na udhalilishaji wa kisaikolojia wa makusudi unaolenga kuponda utu wa binadamu na kufuta kabisa kitambulisho cha mtu binafsi.

Soma zaidi...

Abbas, Akizungumza kutoka Pango la Maadui wa Uislamu jijini Paris, Anathibitisha Dori ya Kihalifu ya Mamlaka ya Palestina katika Kutekeleza Sera za Marekani na Mayahudi Zinazolenga Kufuta Kadhia ya Palestina na Kuwakata Watu wa Palestina na Watoto Wa

Katika mkutano kati ya Abbas na Macron jijini Paris mnamo Jumanne, 11 Novemba 2025, ambapo kuundwa kwa kamati ya pamoja ya Ufaransa na Palestina ya kuandika katiba ya dola ya Palestina kulitangazwa (Al Jazeera Mubasher), Abbas anaonekana kupata msukumo kutoka kwa historia ya dola zilizo katika eneo hili zilizopitisha katiba za Magharibi kama msingi wa sheria zao. Wamewachukua Wamagharibi kama mabwana zao, badala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Abbas hakuweza kufanya chochote ila kugeukia Paris na kuwaomba mabwana zake kuandika katiba ya dola iliyo kwenye karatasi—dola ambayo hawezi kuingia au kutoka bila idhini ya Mayahudi.

Soma zaidi...

Rais wa Slovenia Hajui Historia, au Anaipuuza!

Hii ilikuwa katika mahojiano na Kituo cha Al Jazeera mnamo 9/11/2025, ambayo kituo kilitangaza kikamilifu asubuhi ya 10/11/2025. Kutoka ardhi ya Waislamu huko Qatar, Rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar, anasema: “Israel ina haki ya kuwa na dola.” Swali linaloelekezwa kwa rais ni: Ni nani aliyelipa umbile hili haramu la Kiyahudi haki hii? Na je, kuna mtu yeyote anayesoma historia na hajui jinsi umbile hili lemavu lilivyoanzishwa katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina? Je, mauaji ya Mayahudi dhidi ya Waislamu, watu wa Palestina, yanaondoka akilini mwa msomaji yeyote adilifu wa historia? Umbile hili lemavu lilisimamishwaje juu ya mafuvu na maiti za watu wengi wa Palestina?

Soma zaidi...

Kwa Kuongezeka kwa Ajali za Barabarani, Pindi Uchungaji unapokuwa Haupo na Kubadilishwa na Kulaumu na Kurushiana Lawama!

Mnamo Jumatano, 5 Novemba 2025, ajali mbaya ya barabarani ilitokea katika Barabara ya Al-Arqoub katika wilaya ya Shuqra, jimbo la Abyan, kusini mwa Yemen, ambayo ilisababisha kuchomeka kwa basi la usafiri wa umma lililokuwa njiani kuelekea Aden, likitoka mji wa Jeddah, mali ya Kampuni ya Saqr Al-Hijaz, na lililokuwa limebeba abiria 42.

Soma zaidi...

Amerika, Kutafuta Kuiondoa Darfur, Yaibua Suala la Abyei na Kutishia na Kuonya!

Baada ya kutenganishwa kwa Sudan Kusini na kaskazini mwaka wa 2011, eneo la Abyei liliachwa na utata na kutokuwa la upande wowote — Kusini au Kaskazini — hakukutatuliwa, ilhali kura ya maoni ilitakiwa kufanyika Abyei mwaka wa 2011, sambamba na kura ya maoni ya Sudan Kusini, ili kubaini uhusiano wa eneo hilo na Kaskazini au Kusini, lakini kura ya maoni haikufanyika kwa sababu ya mzozo wa dola hizo mbili kuhusu nani ana haki ya kupiga kura katika kura ya maoni! Eneo hilo linakaliwa na makabila ambayo ni ya Kusini, yaani kabila la Dinka Ngok, na mengine ambayo ni ya Kaskazini, yaani kabila la Misseriya, na bila shaka Wadinka hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kaskazini kwa sababu wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika Dola ya Sudan, na vivyo hivyo Wamisseriya hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kusini kwa sababu wao pia wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika dola hiyo.

Soma zaidi...

Ukumbusho kwa Waislamu kuhusu Utakatifu wa Muislamu: Damu Yake, Mali Yake, na Heshima Yake

Vyombo vya habari vilisambaza habari za uhalifu wa kutisha uliotokea katika mji wa Al-Fashir nchini Sudan, wa mauaji, ubakaji, na uhamishaji uliosababisha maelfu ya familia kuhama. Na swali linalojitokeza ni: je, inawezaje kuwa rahisi kwa Muislamu anayeshuhudia kwamba hakuna mola wa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na anaamini Siku ya Mwisho—inawezaje kuwa rahisi kwake damu ya ndugu yake Muislamu, mali yake, na heshima yake?!

Soma zaidi...

Dharau ya Amerika kwa Raia Wake Yenyewe Yawaacha Wanawake na Watoto na Njaa

SNAP (Programu ya Usaidizi wa Lishe ya Ziada) ni mpango wa shirikisho unaowasaidia watu binafsi, familia, na wale wenye ulemavu kupata manufaa ya kielektroniki ambayo hutumika kwa chakula, vinywaji visivyo na kileo, na mimea kukuza chakula chao wenyewe. Inaripotiwa kuwa kuna Wamarekani milioni 42 ambao hutegemea manufaa ya SNAP kujilisha wao wenyewe na familia zao. 54% ya watu wazima wanaopokea manufaa ya chakula ni wanawake, hasa kina mama wasio na waume, na 39% ni watoto, ambayo ina maana kwamba takriban mtoto 1 kati ya 5 hutegemea manufaa haya ili kuhakikisha hawalali njaa.

Soma zaidi...

Mkuu wa Ujasusi wa Australia Azindua Ulinzi wa Kipumbavu kwa Umbile la Mauaji ya Halaiki

Mkurugenzi Mkuu wa ASIO, Mike Burgess, alitumia hotuba yake ya Taasisi ya Lowy jana kupanua ulinzi wa serikali ya Australia kwa umbile la mauaji ya halaiki. Burgess alitoa mkusanyiko mkubwa wa maneno yaliyopitwa na wakati, yaliyotolewa kutoka kwa serikali na wapigiaji debe wa mauaji ya halaiki, akionya kuhusu vitisho kwa mshikamano wa kijamii, kuongezeka kwa chuki dhidi ya Mayahudi na uhalalishaji wa vurugu za kisiasa. Burgess hata alifikia hatua ya kuonya kuhusu uwezekano wa mauaji ya kisiasa yanayotokana na nchi za kigeni nchini humu.

Soma zaidi...

Mazoezi ya Phoenix Express 2025 Sura Nyingine katika Sura za Utiifu kwa Utawala wa Marekani

Maandalizi ya Tunisia kuandaa toleo jipya la mazoezi ya kijeshi ya pande nyingi, Phoenix Express 2025, katika mwezi huu wa Novemba yanakuja, na hili ndilo zoezi ambalo Komandi ya Marekani ya Afrika imeanza kuandaa kila mwaka baada ya mamlaka iliyopo sasa nchini Tunisia kuihusisha nchi yetu kwa kutia saini pamoja na Marekani, mnamo tarehe 30/09/2020, makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi, ambayo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper aliyataja kama ramani ya utendakazi inayoendelea kwa miaka kumi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu