Jumatano, 17 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/06/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hakuna Mwisho wa Mauwaji kwa Watoto wa Palestina na Lebanon Bila Kuondolewa kwa Umbile la Kiyahudi

Mnamo tarehe 13 Mei, UNICEF iliripoti kwamba angalau watoto 59 waliuawa au kujeruhiwa nchini Lebanon katika wiki iliyopita kutokana na shambulizi la umbile la Kiyahudi nchini humo. Tangu kuanza kwa usitishaji mapigano mnamo tarehe 17 Aprili 2026, angalau watoto 23 wameuawa na 93 kujeruhiwa, na kufikisha jumla ya watoto 200 waliouawa na 806 waliojeruhiwa nchini Lebanon tangu tarehe 2 Machi. Mapema mwezi huu, iliripotiwa kwamba msichana wa miaka 12 na baba yake waliuawa huko Nabatieh baada ya Jeshi la Ulinzi la ‘Israel’ kumlenga kupitia droni kwa mashambulizi matatu ili kuhakikisha kwamba haishi.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Kikao cha Kisiasa

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan ina furaha kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wote walio nah amu na masuala ya umma kuhudhuria kikao kipya cha kisiasa, kinachomkaribisha Ustadh Ibrahim Mushrif, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, chenye kichwa: “Dori Iliyopewa Nchi Jirani katika Vita vya Sudan”

Soma zaidi...

ACSA na GSOMIA: Watu Wenye Ufahamu na Wanasiasa Wenye Ikhlasi Wanapaswa Kujitokeza Kuilinda Nchi Isije Kuwa Nchi ya Kitumwa

Inatisha sana kwa watu wa Bangladesh, wakati vyanzo mbalimbali vinathibitisha kwamba Marekani na Bangladesh zinaendelea na mfululizo wa mikataba ya ulinzi na biashara chini ya ‘Mkataba wa Biashara wa Pamoja (ART)’ wa kikoloni. Kampeni ya Marekani ya GSOMIA ilihama kutoka fahamu dhahania hadi ramani halisi mnamo Machi 2022, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa wakati huo Victoria Nuland alipowasilisha rasimu ya Mkataba Mkuu wa Usalama wa Taarifa za Kijeshi (GSOMIA) ndani ya mfumo wa Mkakati wa Marekani wa Indo-Pacifiki (IPS) ulitarajiwa mnamo 2017 na kuandikwa mnamo 2019. Ingawa ziara ya Nuland ilikuwa alama muhimu kwa GSOMIA, Mkataba wa Upataji na Huduma Mtambuka (ACSA) uliinuliwa rasmi mnamo Aprili 2019 na kuitekelezwa wakati wa Mazungumzo ya 7 ya Usalama jijini Dhaka.

Soma zaidi...

Hali Imefikia Hatua Ambapo Watawala wa Waislamu Wanacheza Kamari na Hatari ya Nyuklia Katikati ya Ardhi za Waislamu!

Afisi ya Habari ya Abu Dhabi iliripoti kwamba timu maalum za kukabiliana na dharura mnamo Jumapili zilidhibiti moto uliozuka katika jenereta ya umeme iliyoko nje ya eneo la ndani la Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Barakah katika eneo la Al Dhafra, kufuatia shambulizi la droni kwenye eneo hilo, bila majeraha yoyote au uvujaji wowote wa mionzi uliorekodiwa. Wizara ya Ulinzi ya Imarati ilieleza kwamba uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha mashambulizi hayo, ikibainisha kuwa maendeleo yoyote yatatangazwa mara tu uchunguzi utakapokamilika.

Soma zaidi...

Enyi Waislamu: Msiruhusu Ardhi Zenu Kuwa Jukwaa la Majeshi ya Wakoloni!

Serikali ya Uingereza imetangaza kupelekwa kwa silaha ya gharama nafuu ya kupambana na droni katika operesheni zake za kijeshi Mashariki ya Kati. Katika taarifa yake, ilisema, “Mfumo mpya sasa umepelekwa katika kumbi za operesheni katika eneo la Mashariki ya Kati.” Pia ilisema kwamba Uingereza “itachangia kwa droni, ndege za kivita, na manuari katika misheni ya kimataifa ili kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz.”

Soma zaidi...

Kilio cha Wafungwa Kinasikika Nyoyoni mwa Waislamu Baada ya Uamuzi wa Umbile la Kiyahudi wa Kutekeleza Taratibu za Unyongaji

Waziri wa Vita na anayeitwa Waziri wa Usalama wa Kitaifa katika umbile la Kiyahudi walitangaza kuanza kwa utekelezaji wa sheria ya adhabu ya kifo kwa wafungwa wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji. Hili lilikuja “baada ya kamanda wa Kamandi Kuu katika jeshi la uvamizi, Avi Bluth, kusaini marekebisho ya amri ya kijeshi inayohusiana na Ukingo wa Magharibi” (Raya Network). Idhini ya Knesset ya uamuzi huo haikutosha kutumia sheria hiyo kwa Ukingo wa Magharibi, ambayo haiko chini ya sheria za kiraia moja kwa moja. Marekebisho haya, yaliyotolewa chini ya amri ya kijeshi, yanaruhusu sheria hiyo kutumika ndani ya mahakama za kijeshi zinazofanya kazi katika Ukingo wa Magharibi.

Soma zaidi...

Mashahidi Watatu Jijini San Diego: Matunda ya Chuki dhidi ya Uislamu

Nyoyo zetu zimejaa huzuni kufuatia mauaji ya kusikitisha ya Waislamu watatu katika msikiti mmoja jijini San Diego wakati wa siku takatifu za kwanza za Dhul Hijjah, miongoni mwa siku takatifu zaidi katika kalenda ya Kiislamu. Familia na jamii zinapojiandaa kwa Idd al-Adha, wakati wa ibada, kujitolea muhanga, na umoja, waumini wasio na hatia badala yake walikutana na vurugu na chuki ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu (swt).

Soma zaidi...

Kama Sehemu ya Kampeni ya “Waislamu Dhidi ya Uhalalishaji Mahusiano” Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon Yafanya Msururu wa Ziara

Kwa kuzingatia mamlaka ya Lebanon kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja ambayo hakika yatapelekea katika amani na uhalalishaji mahusiano na umbile nyakuzi na halifu la Kiyahudi, na kama sehemu ya kampeni ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon kuwatembelea wanasiasa, mamufti, wasomi, nyanja ya kisiasa, na watu mashuhuri, wajumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano na kamati za shughuli za kikanda walifanya ziara. Hizi zilianza katika mji wa Sidon kusini mwa Lebanon kwa ziara ya Mbunge Dkt. Osama Saad, Katibu Mkuu wa Shirika Maarufu la Wananasseristi, na ziara ya Mufti wa Sidon na wilaya zake, Sheikh Salim Sousan. Hii ilifuatiwa na ziara katika mji mkuu, Beirut, kwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Shia, msomi Sheikh Ali Al-Khatib.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Omar Abdel Rahim Khatib (Abu Abdo Khatib)

Kwa kuamini qadhaa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria inamuomboleza kwa Waislamu jumla, na kwa wabebaji dawah haswa, Ndugu Omar Abdul Rahim Khatib (Abu Abdo Khatib), mmoja wa wanachama wake, kutoka kijiji cha Arhab katika vijiji vya magharibi mwa Aleppo, na ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 50, ambayo aliitumia kwa utiifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu