Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Diya')
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa imani kamili juu ya qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kutaka malipo kutoka Kwake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan inaomboleza kwa kuondokewa na mmoja wa wabebaji wake wa Da’wah: Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Diya'), ambaye alifariki dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Alhamisi, tarehe 1 Muharram 1447 H sawia na 26 Juni 2025 M, akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alikuwa na subira na kwa kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu.