Jumanne, 19 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Wito wa Haraka kwa Maafisa na Wanajeshi: Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”

Mnamo Ijumaa, 10 Oktoba 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kuinusuru Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka ambapo ulinganizi ulielekezwa kwa watu wa Tunisia watoe wito wa haraka kwa maafisa na wanajeshi chini ya kichwa, “Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”

Soma zaidi...

Ni Dhambi Kubwa kwamba Gaza Haikukombolewa Au Umbile la Kiyahudi Halikutokomezwa kwa Juhudi za Wanajeshi wa Waislamu, Bali Iliangamizwa Kabisa na Kukombolewa Kidogo kwa Mpango Wa Trump na Usaliti wa Watawala wa Waislamu!!

Serikali ya Misri ilitangaza kusherehekea utekelezwaji wa mpango wa Trump mjini Gaza. Sisi alimwalika Rais wa Marekani kusherehekea kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa mpango wa Gaza: [Rais Trump wa Marekani alisema mnamo Alhamisi kwamba mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru mnamo Jumatatu au Jumanne ya wiki ijayo, na kwamba bado analenga kuzuru eneo hilo kusherehekea hafla hii... “Ni muhimu kutaja kuwa Rais Sisi wa Misri alikuwa amemwalika Trump kushiriki katika sherehe ambazo zitafanywa nchini Misri ili kuadhimisha kutiwa saini kwa makubaliano, akiyachukulia kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo yanazifisha taji juhudi za Misri, Marekani, na wapatanishi katika kipindi cha hivi karibuni.” (CNN Arabic, 9/10/2025)]

Soma zaidi...

Utumiaji kama Silaha wa “Chuki dhidi ya Mayahudi” kunyamazisha Nusra ya Ukombozi wa Palestina

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na mijadala mingi nchini Uingereza ikiashiria kuwepo mafungano kati ya maandamano ya Palestina na kuongezeka kwa chuki dhidi ya Mayahudi na mashambulizi dhidi ya Mayahudi nchini humo. Kabla ya kumbukumbu ya mwaka wa 2 wa shambulizi la Octoba 7 la Hamas dhidi ya umbile la Kizayuni, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, aliwataka wanafunzi wasijiunge na maandamano yanayoiunga mkono Palestina siku hiyo, akionya juu ya “kuongezeka chuki dhidi ya Mayahudi katika barabara zetu”, na kwamba “sio tamaduni ya Uingereza kuwa na heshima ndogo kwa wengine” kwa kufanya maandamano juu ya kumbukumbu hiyo, na kuongeza kuwa maandamano yametumiwa  na baadhi kama “udhuru wa kuchukiza kuwashambulia Mayahudi wa Kiingereza”.

Soma zaidi...

Machozi ya Furaha kwa Maadui wa Mwenyezi Mungu, Kushindwa na Kukata Tamaa kwa Waislamu nchini Cyprus

Aprili iliyopita, Baraza la Mawaziri la Cyprus Kaskazini lilitoa “amri ya kiserikali” ambayo inaruhusu wanafunzi kuvaa hijabu za Kiislamu katika shule za sekondari. Hata hivyo, Muungano wa Walimu wa Sekondari wa Cyprus na Uturuki (KTOEOS), ulianza migomo, ukakataa kufundisha watoto waliofika shuleni wakiwa wamevalia mavazi ya kidini, na hatimaye wakaiomba Mahakama Upeo. Wiki iliyopita (mwisho wa Septemba), Mahakama ya Upeo ya Cyprus Kaskazini ilibatilisha “amri ya kiserikali”, ikiamua kuwa ilikuwa kinyume na katiba. Viongozi wa Muungano huo wa Walimu, ambao waliomba kubatilishwa kwa amri hiyo, walisherehekea kuregea kwa marufuku ya hijabu kama “ushindi kwa usekula” kwa kububujika “machozi ya furaha”. Wakati huo huo serikali imetangaza kuanza mara moja “kufanyia kazi sheria mpya”.

Soma zaidi...

Ulaya Inaendelea Kuunga Mkono Mauaji ya Halaiki mjini Gaza

Licha ya kauli mbiu tupu kuhusu kuitambua dola ya Palestina, Ulaya inaendelea kusafirisha silaha kwa umbile hilo la Kizayuni. Habari zilizovuja zilizopatikana na gazeti la Denmark zinafichua kuwa hivi majuzi mwezi wa Agosti, serikali ya Denmark ilituma vifaa vya silaha kwa ndege zilizotumiwa kuua watoto mjini Gaza.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu