“Siku ya Uhuru” ya 78 Pakistan Itakuwa Huru Kupitia Kuanzishwa kwa Khilafah Rashida
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Chini ya mfumo wa sasa wa kimataifa, kile kinachoitwa uhuru si kitu zaidi ya usanii wa mchezo wa kuigiza, kwan maana ukombozi wa kweli (tahrir) uko pale tu dola inapoweza kupanga mambo yake ya ndani na mahusiano ya nje kwa mujibu wa itikadi yake. Watu wanaoamini “La ilaha illa Allah Muhammadur RasulAllah” kamwe hawatakombolewa kikweli mpaka watabikishe katika ardhi yao mfumo wa Kiislamu wa utawala, uchumi, jamii, elimu, na mahakama, pamoja na sera ya kigeni yenye msingi wa Da‘wah na Jihad. Hii ndiyo maana halisi ya uhuru, na katika suala hili, Pakistan bado haijakombolewa!