Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili jinsia ni Shambulizi dhidi ya Uislamu na Maadili ya Familia. Watawala wa Pakistan, Ni Watumwa wa Magharibi, Wanaotafuta Kuangamiza Kizazi Chetu Kipya
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 5 Septemba 2022, Seneta wa Pakistan Mushtaq Ahmad aliwasilisha mswada wa marekebisho katika Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili Jinsia kwa Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Haki za Kibinadamu. Katika mkutano huo, Seneta Mushtaq Ahmad, alisema kuwa, "‘Transgender’ ni neno la Kimarekani, halina nafasi katika Uislamu, na sheria kuhusu jamii ya watu waliobadili jinsia ni kinyume na Qur'an na Sunnah na itapigia debe ushoga."