Afisi ya Habari
Tanzania
H. 2 Muharram 1447 | Na: 1447 / 01 |
M. Ijumaa, 27 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania Yazindua Kampeni Maalum ya Kulinda na Kutetea Aqida ya Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 2 Muharram 1447 H / 27 Juni 2025 M, Hizb ut Tahrir Tanzania mara baada ya swala ya Ijumaa ilizindua kampeni maalumu ya kitaifa katika Masjid Rahma Buguruni, jijini Dar es Salaam.
Dhamira ya kampeni hiyo ya muda wa miezi miwili ya Hijria (Muharram 1447- Safar 1447 Hijria ni kuilinda na kuitetea Aqida ya Kiislamu.
Kampeni hii imekuja kufuatia kuenea, kuchipuka harakati za kipotofu ambazo hueneza fikra mbali mbali ambazo lengo lake nyuma ya pazia ni kupambana na Uislamu na kutia shaka Waislamu na dini yao.
Kampeni hii ina malengo yafuatayo:
- Kugonga Fikra ya Dini Mseto
- Kugonga Fikra ya Upagani
- Kubomoa Aqeeda ya Dini za Jadi na dini za uafrika
- Kumakinisha Ufahamu Sahihi wa Aqeeda ya Kiislamu kwa upana wake.
Kampeni hii imebeba Kauli Mbiu ya:
“Kataa Dini Mseto, Ukristo, Upagani, Mizimu, baki na Uislamu”
Kampeni itatumia mbinu mbali katika kujitangaza, kufikisha ujumbe wake kwa Umma kama:
- Majukwaa ya wazi ya Kiislamu
- Mihadhara ya wazi na Wakristo na makundi yote mengine yanayobeba fikra dhidi ya Uislamu.
- Uandishi na ugawanyaji wa makala mbali kwa Umma na katika mitandao ya kijamii
- Kuandika na kufikisha nyaraka kwa taasisi na jumuiya mbali mbali zisizo za Kiislamu kuonesha udhaifu wa fikra zao na kufafanua ukweli wa Uislamu
- Kusambaza video fupi fupi katika mitandao ya kijamii.
- Kutumia majukwaa ya Khutba za Ijumaa
- Kutoa taarifa kwa vyombo vya habari
- Kufanya amali za kutangaza kwa mabango (picketing)
- Kufanya vipindi katika TV za mitandao, redio nk.
Hizb ut Tahrir Tanzania inatoa mwito kwa wanajamii kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo. Kwa Waislamu kupata ufafanuzi ziada kwa dini yao. Na wasiokuwa Waislamu watapata fursa adhimu kuutafiti Uislamu kwa hoja na dalili za kiakili.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
https://muslimworld.today/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/tanzania/4753.html#sigProIddad403ce47
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |