Kuunda Kizazi Kitakachopigania Hadhi ya Juu Zaidi Machoni mwa Mwenyezi Mungu (swt) Pekee
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Lengo ambalo Waislamu wanalo kwa kila mtu juu ya matendo yao ni katika kutaka Radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na si chengine. Tunapofunga mwezi wa Ramadhan, tunapotekeleza Swala, kutafuta elimu ya Dini, kuamrisha mema na kukataza maovu, kuhukumu kwa Uislamu, kupigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), kuhifadhi maisha ya wanadamu, kuwalea watoto wadogo wasiojiweza, kuwahudumia wazee...