Ummah Unakua Kiidadi, na Haja ya Khilafah Kusimamisha Dini ni Kadhia Nyeti
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Nimegundua ongezeko la video fupi zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, za watu wakitamka Shahada na kuwa Waislamu. Hilo lilinivutia. Liliniweka kwenye safari ya utafiti ili kujua ni watu wangapi, haswa katika ulimwengu wa Magharibi, wanaokuwa Waislamu. Ni vigumu kukusanya takwimu halisi, lakini Ramadhan 2023 ilishuhudia kusilimu kwa watu mashuhuri.