- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Historia ya Ukoloni wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja wa Sudan
kati ya 1889-2019
(Imetafsiriwa)
Historia ya usuli ya ukoloni wa Sudan ni muhimu kwetu kuielewa, lakini pia historia ya utawala katika eneo la Sudan yenyewe. Imesemekana kuwa Ubeberu wa Uingereza katika karne ya 19 uliunda hali ambazo zimechochea Sudan kugawanyika na kuwa katika mizozo.
Hadi kufikia mwanzoni mwa karne ya 19 eneo hili lilifanya kazi kama msururu wa falme ndogo ndogo ikiwemo Usultani wa Funj na Usultani wa Darfur. Asili ya utawala katika enzi ya Uthmani katika maeneo yasiyo ya mijini haikuwa ile iliyojaribu kudhibiti kila nyanja ya maisha. Hata hivyo, Muhammad Ali Pasha wa Misri alijaribu kuiweka Sudan yote chini ya udhibiti wake katika jaribio lake la kuimarisha mamlaka yake ili hatimaye aweze kujitenga na Uthmaniyya. Sudan ilibaki chini ya udhibiti wa “Misri ya Kiuthmani” hadi karibu 1882.
Waingereza baada ya hapo waliikalia kimabavu na kuikoloni Misri mwaka 1882 na baadaye kukoloni Sudan mwaka 1899. Hii ilitokana kwa kiasi fulani na ushindani mkali wa kibeberu wa Uingereza ilikuwa nao na Ufaransa juu ya ‘kinyang’anyiro cha Afrika’. Kinyang’anyiro cha Afrika kilikuwa ni uvamizi, utekaji na ukoloni wa sehemu kubwa ya Afrika na dola saba za Ulaya Magharibi zilizosukumwa na Mapinduzi ya Pili ya Viwanda mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20 katika enzi ya “Ubeberu Mpya”: Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ureno na Uhispania. Kwa hiyo Waingereza walikuwa na nia ya kupata udhibiti wa Misri na Nile kwa sababu ilikuwa mojawapo ya njia mbili za kibiashara kwa koloni zake nchini India na Afrika Kusini.
Umuhimu wa kimkakati wa Sudan ni dhahiri kutoka kwa jiografia yake. Ni sehemu ya Ukanda wa Mpito wa Afrika/Sahel (neno ambalo linaweza kujumuisha Sudan lakini linatumika zaidi kwa eneo la magharibi mwa bara kuu ikiwemo Niger, Mali, Burkina Faso, Senegal na Guinea), lakini pia ni sehemu ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ujumla zaidi. Pia ni mojawapo ya nchi katika eneo la Bonde la Nile - na ni sehemu ya pwani ya magharibi ya Bahari Nyekundu muhimu kimkakati.
Kwa hivyo, umuhimu wa kimkakati wa Sudan kwa Uingereza na kupata njia za kimkakati za maji kwa maslahi yake ya kiuchumi ndio sababu kuu iliyosababisha uvamizi wa kijeshi wa Sudan mnamo 1898 na vikosi 24,000 vya Anglo-Misri.
Majeshi ya Kibeberu ya Uingereza wakiwemo kina Sir Winston Churchill walipigana dhidi ya jeshi la Khalifa wa Sudan katika vita vya Omdurman. Hii ilihusisha kutekwa kwa mji mkuu wa Khartoum chini ya uongozi wa Anglo-Misri wa Hebert Kitchner. Majeshi ya Anglo-Misri yaliweza kuanzisha kikamilifu uwepo na ushawishi wao ndani ya koloni ya Sudan kupitia hatua ya mikataba kadhaa na sera za utawala zilizoanzisha mamlaka ya pamoja ya Anglo-Misri na Sudan chini ya uongozi wa Mfalme wa Uingereza na Khedive wa Misri. Kinadharia, Misri ilishiriki dori ya kiutawala, lakini kiutendaji muundo wa udhibiti wa pamoja (Condominium) ulihakikisha udhibiti kamili wa Uingereza juu ya Sudan. Magavana na wakaguzi walikuwa maafisa wa kawaida wa Uingereza, ingawa kiufundi walihudumu katika Jeshi la Misri, na watu muhimu katika serikali na utumishi wa umma walibaki kuwa wahitimu wa vyuo vikuu vya Uingereza na shule za kijeshi. Huu hatimaye ukawa utaratibu ambao Uingereza iliidhibiti Sudan hadi kuundwa kwa dola yenye ubwana, na huru ya Sudan mnamo Januari 1, 1956.
Darfur kwa upande mwingine ilivamiwa na kukaliwa kimabavu na Waingereza mwaka 1916, wakiukalia mji mkuu al-Fashir. Sultani wa Darfur, Ali Dinar, alionekana kuunga mkono sana Uthmaniyya wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Tangu wakati huo hadi ‘uhuru’, Darfur ilibakia kuunganishwa na Sudan. Uingereza iliacha udhibiti wa moja kwa moja mwaka wa 1953, lakini mizozo ilifuata kama ilivyokuwa hapo awali wakati Waingereza walikuwa wanaikalia.
Waingereza walidhibiti eneo hilo kupitia njia ya kawaida ya kugawanya na kutawala, kikabila na kidini. Jamii za “Waarabu” zaidi katika kaskazini ziliwezeshwa juu ya jamii za “Kiafrika” zaidi za magharibi na kusini. Watawala wa Uingereza waligawanya nchi hiyo katika kanda mbili tofauti, Kaskazini na Kusini mwa Sudan. Kupitia mchakato unaoitwa ‘Sera ya Kusini’, Sudan Kusini ilitawaliwa tofauti na Kaskazini iliyoendelea zaidi kiuchumi. Ambapo imani za kidini zilikuwepo kusini; Shughuli za kimishonari za Kikristo zilianzishwa. Kwa hivyo, Sudan Kusini ya kisasa ambayo ilijitenga na Sudan mwaka 2011 ni 60% ya Wakristo, 34% ya dini za kiroho, na 6% Waislamu.
Hii ni migawanyiko ya kikabila ambayo imekuwa na makosa katika kipindi cha miongo miwili hadi mitatu iliyopita.
Kulingana na Graham Thomas katika kitabu chake cha 1990 Sudan: Struggle for Survival, “Kuendelea kwa mgawanyiko wa Upande wa Kaskazini kuliimarishwa na uamuzi wa Kitchener kwamba Majimbo ya Kusini yaruhusiwe kugeuzwa kuwa ya Kikristo, huku Sudan Kaskazini ikisalia kuwa ya Kiislamu.” Sera ya Kusini iliambatana na Sheria ya Wilaya Iliyofungwa ya 1922 ambayo ilizuia harakati za watu wasio wa Kusini ndani ya Sudan Kusini.
Kufuatia uvamizi na ukoloni wa Waingereza kuanzia 1896 M hadi 1956 M, miongo iliyofuata ilishuhudia Sudan ikikabiliana na ukoloni wa kisiasa na kithaqafa usio wa moja kwa moja, kuenea kwa maadili mabovu ya kibepari, na mapambano ya ukoloni wa zamani na mamboleo kati ya Uingereza na Amerika.
Sudan kama nchi imekuwa katika hali ya mizozo na ghasia za kudumu tangu uhuru mwaka 1956 hadi leo kupitia uingizaji mkubwa wa silaha ambao umekuza migawanyiko ya kikabila na kisiasa kati ya Marekani na Uingereza.
Marekani hasa, imetumia jeshi kufanya mapinduzi mengi tangu mapinduzi ya Nimeiri mwaka wa 1969. Sudan ilikuwa chini ya ushawishi wa Amerika na muungano mkubwa wa kisiasa na Marekani kuanzia 1972. Rais Jafaar Nimieri alitembelea Marekani mara tano kwa ziara za kibinafsi na ziara moja rasmi ya kikazi kati ya 1979-1985. Alikuwa mmoja tu wa Marais wawili wa Sudan waliotembelea Marekani.
Mnamo 1979, kampuni ya mafuta ya Chevron ya Amerika iligundua akiba za petroli katika Wilaya ya Bentiu ya Upper Nile. Nimeiri ilikanusha umiliki wa kusini wa mafuta hayo wakati huo.
Safari ya mafuta ya Sudan ilianza na kampuni ya mafuta ya Marekani ya Chevron mara tu baada ya vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini vilivyomalizika kwa makubaliano ya amani ya Addis Ababa mwaka wa 1972. Wakati wa Jaffar Nimeri (1969-1985) kama kibaraka wa Marekani, kwa kawaida alikaribisha uhusiano wa kidiplomasia wenye nguvu na Marekani. Mnamo 1982, Sudan ilipokea msaada zaidi wa Amerika kuliko nchi nyingine yoyote katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara – milioni 160 na milioni 100 katika msaada wa kijeshi. Katika ziara ya Nimeiri nchini Marekani mwaka 1983, Ronald Reagan alisisitiza umuhimu wa Sudan chini ya ushawishi wa Marekani ambapo alisema, “Tunapongeza jitihada za Sudan za kuimarisha sekta yake binafsi na kurekebisha sera za serikali zinazozuia maendeleo ya kiuchumi. Maendeleo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa watu wa Sudan na katika jitihada hizi Marekani inafurahia kutoa msaada kwa rafiki.”
Inafahamika vyema kuwa Marekani ilisimamia utekelezaji wa kutenganisha Sudan Kusini mwaka 2011 chini ya utawala wa Obama na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Sudan Kusini. Hii ilikuwa baada ya Marekani kuunda vuguvugu la kujitenga lililoitwa Sudan People’s Liberation Army/Movement (SPLA/M) mwaka 1983, likiongozwa na kibaraka wake, John Garang ambaye alijitahidi kuwadhibiti waasi wote na harakati zao katika harakati moja.
Al-Sadiq Al-Mahdi ambaye alikuwa mkuu wa chama cha National Umma Party alijulikana kwa utiifu wake kwa Waingereza. Aliongoza serikali ya Sudan kati ya 1986 na 1989 na kuondolewa na mapinduzi ya Al-Bashir baada ya hapo. Mnamo 2005, serikali ya Bashir na SPLM/A zilitia saini Mkataba wa Amani Kabambe (CPA). Mazungumzo ya amani yalianza mapema miaka ya 2000 chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo chini ya uongozi wa Kenya, ikiungwa mkono na ‘Troika’ ya Marekani, Uingereza na Norway. CPA ilianzisha dola moja, mifumo miwili ya hukmu, ambapo Kaskazini iliweka sharia huku kusini ikisalia kuwa ya kisekula, na hatimaye ikapelekea uhuru wa Sudan Kusini mwaka 2011. Mwaka mmoja baadaye, Mkataba wa Amani wa Sudan Mashariki (ESPA) ulitiwa saini.
Kwa hivyo, Amerika ndiyo iliyomleta Rais Omar al-Bashir na kundi lake madarakani mnamo 1989 hadi 2019, ili kumakinisha ushawishi wa Amerika nchini humo, na kisha kutekeleza wazo la kuitenganisha Kusini. Kutokana na hayo, Sudan kaskazini pamoja na kusini, zikawa makaazi kamili ya ushawishi wa Marekani.
Hata hivyo, Ulaya, hasa Waingereza kutokana na ushawishi wake katika iliyokuwa Sudan na vibaraka wake nchini humo, waliendelea kujaribu kuingilia kati kila inapowezekana, ili kuregesha ushawishi wake nchini Sudan, au angalau kujaribu kuwa na hisa pamoja na Amerika, hata kama ni kidogo tu.
Kwa mfano, wakati Amerika ilipoanzisha vuguvugu la John Garang la SPLA/M mnamo 1983, Uingereza ilijaribu kuwaingiza wanaume wake katika harakati hii. Katika kipindi hicho, Riek Machar ambaye alikuwa Uingereza akisomea uhandisi wa viwanda na mipango ya kimkakati katika Chuo Kikuu cha Bradford aliregea Sudan kujiunga na SPLA/M. Hata hivyo, wakati huo kulikuwa na mzozo na mapigano kati yake na kiongozi wa SPLA/M John Garang, na kumlazimisha kuondoka katika vuguvugu hilo mnamo 1991.
John Garang alimtuhumu Riek Machar kwa kuwa kibaraka wa Uingereza pamoja na mke wa Riek Machar, Emma McCune ambaye alikuwa Muingereza na amekuwa akifanya kazi chini ya ufadhili wa shirika la misaada la Uingereza/Canada linalofadhiliwa na UNICEF, Street Kids International. Alituhumiwa na John Garang kufanya kazi na Ujasusi wa Uingereza hadi Garang akaviita Vita vilivyotokea kati yake na Machar vita vya Emma. Aliuawa mwaka wa 1993 katika ajali ya barabarani jijini Nairobi. Machar kisha akajaribu kutafuta njia yake ya kujitenga na vuguvugu la Garang na kuunda vuguvugu jengine kati ya mengi yaliyotajwa ya kutaka kujitenga, hasa mwaka 1997 alipoanza mazungumzo na Omar al-Bashir kama mtengaji huru, hata hivyo, alishindwa kufikia hili.
Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Sudan (SPLA/M) Lililoongozwa na Garang liliendelea kubaki kuwa vuguvugu mashuhuri na lenye ushawishi mkubwa na matokeo yake Machar, akishajiishwa na Waingereza, alijaribu kuregea humo. Kwa sababu ya ushawishi mkubwa wa kabila lake la “Nuer”, Amerika ilikubali kurudi kwake ingawa walijua uhalisia wake kuwa ni kibaraka wa Uingereza. Amerika ilimuagiza Garang akubali kuregea kwake ili kumdhibiti chini ya uongozi wake kwa sababu Amerika ilijua uzito wake kutokana na kuwepo kwa kabila nyuma yake, kabila la pili kwa ukubwa kusini. Hata hivyo, tofauti zao katika vuguvugu ziliendelea na Garang akachagua kutomteua kama mtu wa pili katika vuguvugu hilo, lakini badala yake, alimteua Salva Kiir mwenye wadhifa wa chini.
Rais wa sasa wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit ni kibaraka halisi wa Amerika na upinzani wowote dhidi ya uongozi wake umenyamazishwa. Hata hivyo, Riek Machar ambaye alikuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini kuanzia 2011-2013 aliendelea kuwepo katika kile kinachoitwa Sudan People’s Liberation Movement/Army (SPLM/A) kwa nia ya kuwadhibiti na kuwaweka chini ya usimamizi wake, kwa sababu kama wangebakia katika harakati tofauti, basi vuguvugu hizi zilizo nje ya udhibiti wake zingekuwa lango kwa nchi hasimu za Ulaya, haswa Uingereza, na hivyo hili lingekuwa chanzo cha kikwazo kwa miradi ya Amerika.
Kwa hivyo, matatizo mingi ya sasa ya Sudan yanaweza kuonekana kama kukosekana kwa hadhara ya Kiislamu ulimwenguni na katika eneo hilo. Kuna uhusiano wa moja kwa moja na mateso ya wanadamu. Hata hivyo, mustakabali unaweza kuwa chanya. Sio ndoto ya uongo kufikiria Uislamu na Dola ya Khilafah kama suluhisho. Badala yake inapaswa kuwa matarajio ya kweli. Kabla ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuingia Al Madinah, makabila ya Yathrib - Banu Aws na Banu Khazraj - walikuwa katika vita kwa miaka mingi. Makabila mengine katika eneo hilo, kama Banu Nadhir na Banu Quraydhah, yalikuwa yakiwachezea wao kwa wao ili kujinufaisha wao wenyewe.
Lakini kuwasili kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kulibadilisha hilo. Uislamu uliasisiwa kama mfumo. Rehema ikaenea kutoka hapo. Na Mwenyezi Mungu (swt) akatukumbusha tushikamane na Uislamu - Kamba ya Mwenyezi Mungu - na tusifarakane. Kwa sababu mgawanyiko baina yao ulikuwa kama walikuwa ukingoni mwa shimo la moto, lakini wakaokolewa kwa kuasisiwa Muongozo wa Uislamu.
[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ وَاذْكُرُواْ نِعْمَةَ اللّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاء فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىَ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” [Aal-i Imran 3:103]
Sudan imeteseka chini ya ubepari, zaidi ya kuliko wengi. Ilipata ufanisi kwa kila maana chini ya Uislamu - na kwa hakika inaweza kufanya hivyo tena.
#أزمة_السودان
#SudanCrisis
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Tsuroyya Amal Yasna
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir