Jumanne, 18 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/05/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi dhidi ya Ujanja wa Kijeshi wa Marekani katika ardhi ya Tunisia!

Mnamo Ijumaa, 17 Aprili 2026, matembezi yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, yalianza kutoka Msikiti wa Al-Fath jijini Tunis, mji mkuu, baada ya swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yalikuwa na kichwa:

“Ujanja wa Kijeshi wa Marekani kwenye Ardhi ya Tunisia ni Uhalifu.”

Mwanzoni mwa matembezi hayo, ambayo yalihudhuriwa na umati mkubwa wa Watunisia, mmoja wa wanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia aliwahutubia waumini kwa ufupi, akielezea kwamba matembezi hayo yalipangwa kulaani na kupinga ujanja wa kijeshi wa Marekani kwenye ardhi ya Tunisia. Mabango yaliinuliwa, moja likiwa na kichwa cha matembezi na jengine likisomeka, “Ujanja wa Kijeshi wa Marekani nchini Tunisia... Udhalilishaji Huu Utadumu kwa Muda Gani?!” Mabango madogo yalipinga NATO na mengine yakiandikwa “Hapana kwa jeshi la Marekani katika nchi za Waislamu” yaliinuliwa, na waliohudhuria waliimba kaulimbiu katika matembezi yote yaliyozunguka barabara kuu za mji mkuu, wakishutumu ujanja huu, kama vile “Tunisia, Tunisia iko huru, iko huru... NATO nje,” “Tunisia, Tunisia iko huru, iko huru... Amerika nje,” “Tunisia, Tunisia iko huru, iko huru... AFRICOM nje,” “Hapana kwa meli za kivita za Marekani kwenye ardhi ya Tunisia,” “Hapana kwa majeshi ya Makruseda kwenye ardhi ya Tunisia,” “Enyi maafisa na wafanyakazi wa Amerika, mkuu wa ugaidi,” “Enyi maafisa na wafanyakazi wa Amerika, mkuu wa uadui,” “Hapana mola wa haki ila Mwenyezi Mungu... Amerika ni adui wa Mwenyezi Mungu.”

Matembezi hayo yalimalizika katika Barabara ya Al-Thawra mbele ya Ukumbi wa Manispaa kwa mkutano ambapo mwanachama mmoja wa Hizb ut Tahrir/Tunisia alitoa hotuba. Alisema, “Njia hizi za kijeshi za Marekani zinazofanyika katika ardhi ya Tunisia si tukio la kupita tena au ushirikiano mdogo wa kiufundi. Badala yake, kupitia marudio na upanuzi, zimebadilika kuwa urekebishaji wa vitendo wa uwepo wa jeshi la Marekani, na kufikia kilele cha Tunisia kuandaa mazoezi makubwa zaidi ya ‘Simba wa Afrika’ mwaka wa 2025! Majeshi ya Marekani, yanapoingia katika nchi, huiharibu na kuwadhalilisha watu wake, na hivi ndivyo wanavyofanya. Uhalifu wao nchini Iraq na Afghanistan unashuhudia hili, na usaidizi wao usio na kikomo kwa umbile la Kizayuni katika mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza unajulikana sana. Tunawezaje, baada ya haya yote, kumruhusu adui katili, ambaye hajali agano au wajibu wowote, kukanyaga ardhi yetu, ardhi ya kijani kibichi, ardhi ya mujahidina, wakati Mwenyezi Mungu asema, ‘Na Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia [ya mamlaka] juu ya waumini’? Wajibu wa watu wa nchi hii leo, na wajibu wa wale walio na nguvu na ulinzi, ni kukata mikono ya Magharibi kutoka katika ardhi zetu, hasa kichwa cha nyoka, Amerika, kwani yeye ndiye adui wa kihakika wa Uislamu na Waislamu. Hilo linaweza kupatikana tu kwa kukataa mbinu hizi na kufuta makubaliano ya kijeshi yaliyosainiwa na Beji Caid Essebsi. Makubaliano haya ni uovu mkubwa ambao utakuwa na athari kubwa kwa eneo hili na uhuru wake. Lazima pia mufanye kazi ili kusimamisha dola yenye nguvu na ya kifahari ndani ya mradi wa kihadhara unaotokana na aqida ya umma, ambao unatoa mamlaka kwa umma na ubwana kwa sheria ya Kiislamu, na kuondoa uwepo wa kikoloni kwa majeshi yenye nguvu ambayo yanalinda mujtamaa wa Waislamu na kunyamazisha minong'ono ya Shetani kutoka kwa maadui wa dini. Kwa njia hii, heshima ya nchi na usalama na uhuru wa taifa vitahifadhiwa.

Hii ndio kazi ya Hizb ut Tahrir katika nchi ya mzeituni. Huu ndio wajibu wake kwa umma wake na wale walio katika nafasi za madaraka: kufichua mipango na hila za mkoloni kafiri anayefanya kazi bila kuchoka ili kuimarisha mshiko wake kwenye ardhi za Waislamu na kuzuia jaribio lolote la ukombozi kutoka kwenye magereza yake—“vizimba vya Sykes-Picot”—ili tuendelee kuwa taifa nyenyekevu, lililotiishwa, na lililodhalilishwa. Inaendelea na kazi yake pamoja na wenye ikhlasi hadi itakapovunja minyororo hii, kuikata mikono ya Amerika na washirika wake katika nchi za Waislamu, na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kama alivyoitolea bishara njema kiongozi wetu Muhammad (saw), aliposema: ثم تكون خلافة على منهاج النبوة “... kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Ijumaa, 30 Shawwal Al-Khair 1447 H – 17 Aprili 2026 M

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu