Alhamisi, 05 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ubwana Unaofifia: Mpango Mpya wa Mafuta wa Pakistan, Vita vya Kale na Sera ya AI

(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah – Toleo 562 - 27/08/2025 M

Na Abdul Majeed Bhatti

Mnamo Julai, Rais Trump wa Amerika alichapisha kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Jamii. “Hivi punde tumemaliza mkataba na nchi ya Pakistan, ambapo Pakistan na Marekani zitafanya kazi pamoja katika kuendeleza hifadhi yao kubwa ya mafuta.” [1] Mkataba wa mafuta ni sehemu ya mkataba mpana wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ambapo Marekani imekubali kupunguza ushuru kwa bidhaa za Pakistan kutoka 29% hadi 19%, huku ikitishia kuweka ushuru wa adhabu kwa India, isipokuwa New Delhi imalize uagizaji mafuta ghafi kutoka Urusi. Inashangaza, mara tu baada ya mpango huo, kampuni kubwa zaidi ya kusafisha mafuta ya Pakistan, Cnergyico, ilitangaza mipango ya kuagiza mapipa milioni 1 ya mafuta ghafi ya Marekani, kuashiria mabadiliko kutoka kwa utegemezi wake wa jadi kwa wasambazaji wa mafuta wa Mashariki ya Kati. Hii inasisitiza juhudi kubwa za Pakistan za kuuridhisha utawala wa Trump sio tu kwa mafuta bali pia sekta zengine. Wizara ya Fedha ya Pakistan iliusifia mpango huo kama “mwanzo wa enzi mpya ya ushirikiano wa kiuchumi, haswa katika nishati, migodi na madini, IT, sarafu ya crypto, na sekta zengine.” [2]

Uchunguzi wa karibu wa mkataba huo wa mafuta unaonyesha kuwa uongozi wa nchi hiyo hauoni ubaya katika kupoteza rasilimali na ubwana wa eneo la Pakistan ili kuifurahisha Washington. Amerika itapata njia isiyo na kikomo ya kuyanyonya—huko Baluchistan ikiwa na matarajio ya ziada huko Sindh, Punjab, na Khyber Pakhtunkhwa—akiba ya mafuta ambayo haijatumiwa. Huenda hili likamaanisha mwisho wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC) na kuharakisha mradi mpya wa Mashariki ya Kati wa Amerika, ambao unalenga kuzifanya Iran, Afghanistan na Pakistan kuchora upya ramani na kuzaa nchi mpya na tawala tiifu kwa Amerika. Zaidi ya hayo, ikiwa mafuta yatawahi kunyonywa, walengwa wakuu watakuwa makampuni ya mafuta ya Marekani na wanakandarasi ambao watarejesha mali ya Pakistan iliyofichwa kama punguzo la kodi ili kuimarisha uchumi wa Marekani. Mafuta ya Pakistan hayabaki tena kuwa mali ya kimkakati ya kutumikia maslahi ya Wapakistan; sasa ni bidhaa ya kibiashara iliyo chini ya huruma ya Amerika.

Kuuacha ubwana na uhuru wa Pakistan kwa badali ya kuisinga ghera ya Trump ni alama kuu ya uongozi wa kijeshi na kiraia wa nchi hiyo. Katika vita vifupi na India, ambapo Pakistan ilikuwa na mkono wa juu, viongozi walipoteza fursa nzuri ya kutatua masuala ya kudumu ya nchi. Mizozo ya maji inayotawaliwa na Mkataba wa Maji wa Indus (IWT) bado haijatatuliwa, Kashmir inaendelea kukaliwa kimabavu, na CPEC-kiini kinachodhaniwa cha ufufuo wa uchumi wa Pakistan-inazidi kutokuwa thabiti kwa sababu ya mivutano ya mipakani. Badala ya kudai uhuru wa kimkakati, Islamabad ilimsihi Trump kuingilia kati na kisha kumteua kwa tuzo la Amani la Nobel. Hii inaiacha Pakistan tena kwa huruma ya India kwa maji yanayohitajika sana kukuza mazao na kulisha idadi yake inayoongezeka kwa kasi. Zaidi ya hayo, nchi lazima iweke idadi kubwa ya wanajeshi katika nafasi za ulinzi kando ya Mstari wa Udhibiti (LoC), ikikamua rasilimali na kuweka jeshi zaidi eneo hilo bila kupata suluhisho la maana kwa ukosefu wake wa usalama wa muda mrefu na India. Ukosefu huu wa mtazamo wa kimkakati na utegemezi unaoendelea kwa Marekani unakanusha madai yoyote Pakistan huru.

Hata sekta ya teknolojia yenye mustakabali mzuri ya Pakistan – licha ya talanta yake kubwa – haijasazwa kutokana na makubaliano ya ubwana yaliyowekwa na uongozi wa nchi. Sera ya kitaifa ya AI iliyotangazwa sana, ingawa ni kabambe kwa sauti, inaonyesha utegemezi wa kina wa teknolojia, majukwaa na ushirikiano wa kigeni kutoka nje. Bila juhudi za dhati za kuunda hesabu za ndani, vituo vya data, na algoriti huru, Pakistan inahatarisha kuwa mtumiaji wa mifumo ya kigeni ya AI badala ya mzalishaji. Sera hiyo inazungumza lugha ya uvumbuzi, lakini katika hali yake ya sasa, inaimarisha utegemezi kwa makampuni makubwa ya teknolojia ya Marekani na China, na kuiacha Pakistan bila udhibiti wa ile mifumo ambayo itaunda utawala wake, uchumi na ulinzi katika miongo kadhaa ijayo.

Katika hali mithili ya hiyo, Sheria ya Mali isiyohamishika ya 2025, na Baraza la Crypto la Pakistan sio zaidi ya pazia la kufanya kazi na kampuni za crypto zinazonasibishwa na Rais Trump. [3] Bado, wanufaikaji wakuu wa mpango wa sarafu ya crypto wa Pakistan ni kampuni za Marekani na Rais Trump, huku Wapakistani wa kila siku wakivumilia kukatika kwa umeme na uhaba wa maji huku rasilimali chache za nchi hiyo zikielekezwa kwenye kampuni za crypto zenye ulafi wa nishati ya mafuta zinazofungamanishwa na maslahi ya Trump.

Katika nyanja zote tatu—nishati, Kashmir inayokaliwa kimabavu, na teknolojia—Pakistan inapendelea maslahi ya Marekani badala ya ubwana wake. Inasalimisha utajiri wake wa asili kwa makampuni ya Marekani, mafanikio yake ya kimbinu yaliyopiganiwa sana dhidi ya India ili kumwinua Trump kama mweka amani na mustakabali wake wa kidijitali kwa majukwaa ya Marekani. Bila marekebisho ya kimsingi ya mwelekeo, uongozi wa Pakistan utaiangamiza nchi hiyo.

Kwa hivyo, Waislamu wa Pakistan lazima wachukue jukumu lao wenyewe kuzuia mfumo huu mbovu unaoongozwa na viongozi ambao madhumuni yao ni kumridhisha mbeberu Trump. Hili linaweza kufikiwa tu kwa kusimamishwa tena Dola ya Khilafah Rashidah.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Maregeleo

[1, 2] Janjua H., (2025). Why are the US and Pakistan making an oil deal? DW. Available at: https://www.dw.com/en/why-are-the-us-and-pakistan-making-an-oil-deal/a-73498835

[3] The Pakistan Code, (2025). Available at:https://pakistancode.gov.pk/english/UY2FqaJw1-apaUY2Fqa-apaUY2Npa5tlbA%3D%3D-sg-jjjjjjjjjjjjj

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu