Katiba za kutungwa na Wanadamu ni rahisi kukengeukwa na kubadilishwa
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mahakama ya Upeo imetoa uamuzi wa kuusambaratisha mradi wa ujenzi wa madaraja lakini ikafungua dirisha kwa vinara wa makubaliano ya ‘handshake’ kuanzisha marekebisho mpya ya kikatiba. Kwenye uamuzi wake wa kihistoria, siku ya Alhamisi 31 Machi, 2022 jopo la majaji saba lilibatilisha hoja tano za mahakama ya rufaa zilizotumia kupinga mabadiliko ya kikatiba kama yalivyopendekezwa na mradi wa BBI.