Al-Waqiyah TV: Shikamaneni na Agano la Mwenyezi Mungu (swt), Iman na Nusrah (Usaidizi wa Kijeshi)!
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Shikamaneni na Agano la Mwenyezi Mungu (swt), Iman na Nusrah (Usaidizi wa Kijeshi)!
Shikamaneni na Agano la Mwenyezi Mungu (swt), Iman na Nusrah (Usaidizi wa Kijeshi)!
Jibu kwa Kongamano la Suluhisho la Dola Mbili!
Hizb ut Tahrir/Denmark iliandaa kikao, mbele ya ubalozi wa Misri katika mji mkuu wa Copenhagen cha kuwanusuru na kuwaombea nusra watu wetu mjini Gaza na Palestina yote inayokaliwa kwa mabavu, kutoka mto wake hadi bahari yake. Ustadh Abdul Rahman Muhammad, mwanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Denmark, alitoa kalima kwa waliohudhuria.
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia ilifanya matembezi makubwa katika mji mkuu wa Tunis, mbele ya Msikiti wa Al-Fath baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 25 Julai 2025 M chini ya kichwa: “Serikali za Kijamhuri na za Kifalme Zimeisaliti Gaza... Kwa Khilafah tutainusuru Gaza”
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (ra) kuwa amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “Hajaamini yule ambaye analala tumbo lake likiwa limeshiba na hali ya kuwa jirani yake ana njaa na yeye anajua.” Basi vipi kuhusu mji wa Gaza ambao watu wake wanakufa njaa, huku pambizoni mwake kuna ardhi zilizo jaa neema na kheri nyingi, chini ya utawala wa watawala walioisaliti, na kula njama dhidi yake pamoja na maadui zake, wakafunga mipaka na kuziba midomo ya wale walioomba msaada na nusra. Hawakuridhika na kuisaliti tu, walizuia nusra yake na wakajitahidi kuizingira, wakiinyima chakula na dawa.
Katika onyesho la wazi la ukosefu wa usalama na unafiki, serikali inayoitwa ya “kidemokrasia” ya India, chini ya utawala wake wa kibaniani wa BJP, imetoa amri ya kupiga marufuku vitabu 25 vinavyoandika uhalisia wa kihistoria wa ukaliaji wake wa kimabavu wa Kashmir. Hatua hii, ya tarehe 5 Agosti 2025, inatoka kwa Idara ya Mambo ya Ndani ya idara wa Jammu na Kashmir, ikitangaza kwamba kazi hizi “feki” chini ya Kifungu cha 98 cha Bhartiya Nyaya Sanhita 2023, ikizituhumu kwa kueneza “simulizi za uwongo”, kupigia debe kujitenga, na kutukuza “ugaidi”.
Vijana wawili wametoweka baada ya video yao kusambaa mitandaoni inayoonyesha wakivamia kituo cha polisi katika makao makuu ya Usalama wa Dola katika kituo cha polisi cha Ma’asara huko Helwan kusini mwa Cairo, ambapo waliwaweka wanausalama kwenye seli ya gereza. Kusudio la hatua hii ilikuwa kupinga utepetevu wa maafisa kwa watu wa Gaza.
Bunge la Seneti la Uzbekistan limeidhinisha sheria inayotoa adhabu ya uhalifu kwa kufundisha watoto dini bila kibali na elimu ifaayo. Vitendo kama hivyo sasa vinaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka mitatu gerezani.
Umbile la Kiyahudi bado linatekeleza uhalifu wake dhidi ya watu wa Gaza, hivyo makumi ya mashahidi huongezeka kutokana nao kila siku. Pia bado linapiga mzingiro wake juu ya Gaza, hivyo watu wake wanakufa kwa njaa, kwa kuwa hawana chakula, vinywaji, dawa, au makao, licha ya jitihada fulani za kupeleka misaada kwao kwa uoga! Lakini mamia ya maelfu hawapati tonge ambalo kwalo wanaweza kuzuia njaa zao au kunyamazisha njaa ya watoto wao, kwa hiyo wamekuwa wanakufa kwa njaa mbele yao na mbele ya macho ya ulimwengu wote bila msaidizi au mwenye kuwanusuru.
Wakati sera ya mauaji ya halaiki na njaa huko Gaza ikiendelea huku ukatili wake wote ukionekana na kusikilizwa na dunia nzima, Uturuki vile vile, inaendelea na hatua zake rasmi za kukabiliana na ongezeko la misimamo ya rai jumla nchini Uturuki. Hata hivyo, haikutia saini taarifa iliyotayarishwa na The Hague Group huko Bogotá, mji mkuu wa Colombia, Julai 15–16. Lakini katika kujibu majibu hayo, Wizara ya Mambo ya Nje ilidai kuwa taarifa hiyo huenda ikatiwa saini hadi Septemba 20, na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan alitangaza kuwa wana dukuduku katika muktadha wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari.