Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 552
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katikati ya angahewa Amerika inaenea katika eneo hili kupitia kwa rais wake Trump, akitoa wito wa amani na Mayahudi, na kwa mujibu wa Makubaliano ya Abraham yaliyokuja wakati wa ziara yake ya kuchukiza katika eneo hilo, na kujisalimisha kwa watawala wa Kiarabu na Waislamu kwenda sambamba na ajenda hii, hadi kufikia kiwango ambacho mbora zaidi kati yao anaweza kusema ni "tutakuwa wa mwisho kuhalalisha mahusiano na Mayahudi", katika muktadha huu wa Mahojiano Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam wakati wa mahojiano na Mtandao wa CNN, yaliyochapishwa mnamo 30/5/2025, ambapo alisema: "Uhalalishaji mahusiano ni sehemu muhimu ya amani tunayotaka kuona kesho, sio kesho kutwa!"
Wakati Tanzania ikitarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, wimbi la mgawanyiko wa kisiasa na mitazamo tofauti kuelekea uchaguzi huo lipo miongoni mwa wanasiasa na vyama vya kisiasa ambalo limezua mjadala mkubwa wa kisiasa.
Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa la Kijamii la ‘Truth’: ["Iran na Israel wanapaswa kufanya makubaliano, na watafanya makubaliano, kama vile nilivyozifanya India na Pakistan kufanya." Aliendelea: "Vivyo hivyo, tutakuwa na AMANI, hivi karibuni, kati ya Israel na Iran! Miito mingi na mikutano inafanyika hivi sasa."(Sky News,15/6/2025). Mnamo Jumapili, msemaji wa jeshi la umbile la Kiyahudi alisema kupitia jukwaa la X kwamba "Israel ilitoa onyo kwa Wairan wanaoishi karibu na vinu vya nyuklia nchini Iran kuhama makaazi yao." Wakati huo huo, msemaji wa jeshi la 'Israel' alisema kuwa jeshi lilishambulia kituo cha nyuklia katika mji wa Isfahan, katikati mwa Iran. Tangu alfajiri ya Jumapili, Iran ilianza kurusha raundi mpya za makombora kwenye shabaha ndani ya 'Israel', na kusababisha vifo na makumi ya majeruhi, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa nyumba na majengo. Kwa kujibu, Tehran imekuwa chini ya mashambulizi ya 'Israeli'. (Al Jazeera,15/6/2025).
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (Médecins Sans Frontières) limeonya kuwa wanawake na wasichana katika jimbo la Darfur nchini Sudan wako katika hatari ya karibu kila mara ya unyanyasaji wa kijinsia. Mizani halisi ya mgogoro huu inasalia kuwa vigumu kubainisha, kwani huduma bado ni chache na watu wanakabiliwa na vikwazo katika kutafuta matibabu au kuzungumza kuhusu masaibu yao. Hata hivyo, manusura wote waliozungumza na timu za MSF huko Darfur na kuvuka mpaka nchini Chad walisimulia hadithi za kutisha za ghasia za kikatili na ubakaji. Huku wanaume na wavulana pia wakiwa hatarini, kiwango cha mateso kinapita maelezo.
Meli ya misaada ya "kwenda Gaza" ya Madleen na matendo ya wanaharakati wake maarufu wasio Waislamu yamekuwa na athari kubwa kwenye vyombo vya habari vya kawaida na mitandao ya kijamii. Nchi nyingi, ikiwemo Uturuki, zilitoa "msaada wa ushauri" kwa raia wao wenyewe kwenye meli hiyo, ambayo ilikamatwa na umbile vamizi la kigaidi la kizayuni.
Katika mandhari inayojirudia rudia, kwa kila maafa yanayowakumba watu waliozingirwa wa Gaza, tawala za Kiarabu - zinazoongozwa na utawala wa Misri - zinathibitisha kwamba sio tu hazipo katika wajibu wao wa kunusuru, lakini pia ziko katika nafasi ya ulaji njama na usaliti, na hata kushiriki kikamilifu katika mzingiro, kulinda vivuko na kuzuia mradi wowote wakilishi au maarufu kwa lengo la kukandamiza Waislamu.
Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa alikutana na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, katika mji mkuu wa Saudi, Riyadh, mnamo Jumatano, kando ya mkutano wa kilele wa Ghuba na Marekani. Mfalme matarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman alihudhuria mkutano huo, huku Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan akishiriki kwa njia ya video, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudia.
Mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na Kamati ya Amani ya Kiraia katika jengo la Wizara ya Habari jijini Damascus mnamo Jumanne, Juni 10, 2025, chini ya uenyekiti wa mwanakamati Hassan Soufan, ulizua wimbi kubwa la hasira na chuki kubwa miongoni mwa Wasyria, hasa miongoni mwa familia za mashahidi na waliopotea, na watoto wa mapinduzi. Wengi waliona kauli za mkutano huo kama uchochezi kwa familia za wahasiriwa, kupuuza mihanga ya wanamapinduzi, kudharau damu ya mahsahidi, kukana ukweli usiopingika, na uhalalishaji wa wazi wa wahalifu wa kivita. Hafla hiyo ilionekana kama jaribio la kulalalisha mahusiano kwa nembo za utawala ulio ng’atuliwa chini ya mabango ya "amani ya raia," "kujenga taifa," na "kuzuia umwagaji damu."
Mnamo siku ya Ijumaa, tarehe 13/6/2025, alfajiri, umbile la Kiyahudi lilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran, yakilenga vituo vyake vya nyuklia, viwanda vyake vya makombora ya balestiki, na viongozi wa kijeshi, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa maisha na mitambo ya kijeshi na ya kiraia, kwa msaada na ushirikiano wa Marekani. Iran, kama kawaida, iliapa kutoa jibu kali na baya kwa umbile la Kiyahudi kupitia mashambulizi ya droni na makombora. Ilitekeleza mawimbi ya mashambulizi haya asubuhi na jioni ya siku hiyo hiyo, yakivuka anga ya Iraq, Syria, na Jordan. Baadhi ya mashambulizi haya yalisababisha uharibifu kwa baadhi ya vifaa katika miji ya umbile hilo, kabla ya baadhi yake kupanguliwa katika anga ya jirani kabla na baada ya kufika kwenye umbile la Kiyahudi.