Sio Taarifa ya Bogotá wala Tangazo la New York litaweza kuliokoa umbile la Kiyahudi!
- Imepeperushwa katika Uturuki
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wakati sera ya mauaji ya halaiki na njaa huko Gaza ikiendelea huku ukatili wake wote ukionekana na kusikilizwa na dunia nzima, Uturuki vile vile, inaendelea na hatua zake rasmi za kukabiliana na ongezeko la misimamo ya rai jumla nchini Uturuki. Hata hivyo, haikutia saini taarifa iliyotayarishwa na The Hague Group huko Bogotá, mji mkuu wa Colombia, Julai 15–16. Lakini katika kujibu majibu hayo, Wizara ya Mambo ya Nje ilidai kuwa taarifa hiyo huenda ikatiwa saini hadi Septemba 20, na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan alitangaza kuwa wana dukuduku katika muktadha wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari.