Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 3 Rabi' II 1448 | Na: H 1448 / 043 |
| M. Jumanne, 15 Septemba 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuelezea tu Uchokozi na Maovu ya Umbile la Kiyahudi dhidi ya Eneo hilo Hakutalizuia wala Kukomesha Matamanio yake
(Imetafsiriwa)
Tumeona jinsi adui wa Mwenyezi Mungu, Netanyahu, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, alivyojigamba siku chache zilizopita kuhusu udhibiti wake wa eneo hilo, akisema wakati wa kuingia Mwaka Mpya wa Kiyahudi: “Tuko juu ya Mlima Hermon. Damascus hii hapa, Lebanon hii hapa, Milima ya Golan ya Syria hii hapa, na tunadhibiti eneo lote kuanzia Kilele cha Hermon hadi Mto Yarmouk, na kutoka hapa hadi Bahari ya Mediterania – udhibiti kamili ambao haujawahi kuonekana hapo awali.”
Kwa upande mwingine, yale aliyoongeza Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, mnamo Jumapili, katika mkutano wake wa pamoja na mwenzake wa Syria, Asaad al-Shibani, yalikuwa ni kulituhumu umbile la Kiyahudi kwa kujaribu kuvuruga utulivu wa Syria na kuendelea kukwamisha kile alichokiita mwelekeo chanya ambao nchi hiyo inaupitia; huku al-Shibani akisisitiza msimamo wa Damascus wa kutumia njia ya kidiplomasia katika kukabiliana na hali hiyo inayozidi kuwa mbaya. Fidan alisema: “Kama vile Syria inavyotoa matumaini makubwa kwa eneo hili na dunia, ghafla kuna mhusika anayejitahidi kuvuruga utulivu wa nchi hiyo,” akaongeza, “Mnafahamu jina la mhusika huyo: ‘Israel’.” Huku akitaja shambulizi la anga dhidi ya kambi ya jeshi la anga ya Abu al-Duhur kaskazini-magharibi mwa Syria mwezi uliopita kama mfano wa hivi karibuni wa jambo hilo.
Basi, nini kinafuata baada ya mawaziri wote wawili kutambua uhalisia wa umbile la Kiyahudi, dori zake, na uchokozi wake?!
Hakika, uhalisia kwamba umbile la Kiyahudi ni umbile lenye tabia kama ya saratani linalopanua na kueneza ufisadi katika eneo hili hauhitaji wataalamu, mabingwa, na maafisa ili kuutambua; kwani ni jambo lililo wazi mno kiasi kwamba haliwezi kufichika machoni wala kupotea akilini mwa mtu. Na eneo hili halihitaji mtu wa kulibainishia ugonjwa na janga lililolipata kutokana na uhalifu na matamanio ya Mayahudi; bali linahitaji mtu wa kukomesha mambo hayo na kulikomboa kutoka kwao na maovu yao.
Kwani uchokozi wa umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wetu huko Gaza umeshuhudiwa na dunia nzima, na ni uchokozi ambao dunia haijawahi kushuhudia mfano wake kwa miongo kadhaa. Na uchokozi wake dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, Ukingo wa Magharibi, Lebanon, Syria, Yemen, Iran, na Iraq haujakoma, huku tishio lake la kuilenga Misri na Uturuki baada ya Iran likiwa limejulikana. Na isipokuwa jeshi kutoka miongoni mwa majeshi ya Waislamu—kama vile jeshi la Uturuki, Misri au mengineyo—liinuke dhidi ya umbile hili vamizi, basi Mayahudi na azma yao ya kuwa na dola kati ya mito hiyo miwili havitakoma.
Uchokozi wa Mayahudi uko wazi, kiburi chao kimevuka mipaka yote, uhalifu wao umefikia kilele cha juu kabisa, na ndoto zao za upanuzi wa himaya zimefichuka. Hili ni suala ambalo mikutano ya waandishi wa habari na masuluhisho ya kidiplomasia sio stahiki kulishughulikia; badala yake, hatua madhubuti zinahitajika ili kuliondolea eneo hii na Umma maovu yake. Majeshi ya kwanza yanayostahiki heshima hii ni wanapinduzi wa Ash-Sham—wale waliomwangusha dhalimu wa Ash-Sham kwa azma yao na mikono yao safi—pamoja na kizazi cha Sultan Abdul Hamid wa Pili, Muhammad al-Fatih, Suleiman al-Qanuni, na Makhalifa wengine wema wa Nasaba ya Kiuthmani, ambao walilinda ngome ya Uislamu na ardhi za Waislamu kwa miongo mingi na mirefu.
Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [Surah At-Tawbah: 38].
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) muslimworld.today |



