Jumanne, 10 Rabi' al-thani 1448 | 2026/09/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  6 Rabi' II 1448 Na: 1448 / 03
M.  Ijumaa, 18 Septemba 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ahadi na Matumaini ya Serikali ya Iraq ni kama Mangati (Sarabi) ambayo Mwenye Kiu Huiona kuwa ni Maji!
(Imetafsiriwa)

Baada ya Marekani kusisitiza kumweka Ali Al-Zaidi kama Waziri Mkuu wa Iraq na kumuunga mkono, huku ikimkataa mgombea wa Muungano wa Uratibu (Coordination Framework), Nouri al-Maliki, na kutishia kuweka vikwazo vya kiuchumi, na baada ya jambo hilo kufanikiwa kama ilivyotaka, ilifanya hatua kadhaa za kuboresha taswira yake na kuwashawishi wananchi wa Iraq kuwa yeye ndiye mtu sahihi kwa wakati huu, na mwenye uwezo wa kuiokoa Iraq na kuifikisha mahali salama. Hivyo, ilimwalika Washington kutangaza kuanza kwa awamu mpya kuhusu uchumi wa Iraq, jambo ambalo alianza kwa kampeni ya kuwawajibisha mafisadi. Afisi yake ya habari ilieleza katika taarifa iliyoripotiwa na Al Jazeera kwamba: "Jumla ya mikataba 48, hati za makubaliano, mikataba ya ushirikiano, na matangazo ya ushirika vilisainiwa kati ya taasisi za sekta ya umma na binafsi nchini Iraq na Marekani." Taarifa hiyo iliongeza kuwa mikataba hii inajumuisha "ushirikiano na ushirika unaohusisha wizara za mafuta na umeme... pamoja na makampuni ya ExxonMobil, KBR, GE Vernova, Shell na Halliburton", pamoja na makubaliano kadhaa yanayohusiana na ujenzi wa bomba kubwa la mafuta ghafi kati ya Iraq na Syria.

Mambo haya yaliwekewa sharti la kupokonywa silaha kwa makundi ya Iraq yanayoungwa mkono na Iran, kabla au kufikia tarehe 30/9/2026, ili hatua hiyo iendane na tangazo la kuondoka kwa majeshi ya Marekani kutoka Iraq.

Lakini uhalisia unaoshuhudiwa unaonyesha kuwa ahadi za kuijenga Iraq na kuiregesha kama dola imara na yenye mamlaka kamili si chochote ila ni uongo na udanganyifu. Marekani haijali chochote isipokuwa maslahi yake yenyewe, wala haijali nchi nyingine, hata kama zitaangamia katika hali mbaya kiasi gani. Nchi hizi za Ghuba zinalipia gharama ya utegemezi wao katika vita vya Marekani dhidi ya Iran, huku Marekani haifanyi lolote kuwalinda au kuwatetea, licha ya kwamba kila wanachokipitia kinatokana na sera na vitendo vyake!

Enyi Waislamu: Baada ya kelele hizi zote na ahadi hizi za uongo, tunaona kuwa hali ya Iraq imekuwa mbaya zaidi kuliko hapo awali. Uhitaji, umaskini, ukosefu wa ajira, na kupanda kwa bei vimefikia kiwango kisichovumilika, na kila mwezi serikali inaingia katika mgogoro kuhusu mishahara ya wafanyikazi na jinsi ya kuipata; wakati mwingine ni mgogoro wa gesi ya kupikia, na wakati mwingine ni mgogoro wa mafuta ya magari... Hivyo, ni maisha gani ya raha wanayowaahidi?!

Je, haitoshi kuwafanya muwe kama walioleweshwa na kukimbiza ndoto zisizo na uhalisia na taswira za udanganyifu?! Je, haitoshi kwamba mumeumwa mara kwa mara kutoka kwenye shimo moja, huku mukikumbuka onyo la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «لا يُلدَغُ المُؤمِنُ مِن جُحرٍ واحِدٍ مَرَّتَينِ» “Muumini haumwi kutoka kwenye shimo moja mara mbili.

Je, bado hamjatambua kwamba wokovu wenu na urekebishaji wa hali yenu unaweza tu kupitia kwa mikono yenu wenyewe na si kupitia mikono ya maadui zenu?! Kwani nyinyi ni Umma unaomiliki mfumo mtukufu kabisa wa maisha, ambao Mola wa watu ameuweka na akakuamrisheni kuutekeleza katika uhalisia wa maisha. Ni heshima na ukumbusho. Amesema Mwenyezi Mungu (swt): [لَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَاباً فِيهِ ذِكْرُكُمْ أَفَلَا تَعْقِلُونَ] “Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?” [Surah Al-Anbiya: 10]. Na akakutahadharisheni dhidi ya kujiepusha nayo kwa maisha ya dhiki. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى] “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surah Ta-Ha: 124]. Nendeni kwenye kazi nzito na ya dhati ya kusimamisha Khilafah na mutabikishe Shariah ya Mwenyezi Mungu, jambo ambalo Hizb ut Tahrir imeendelea kukulinganieni kwalo. Je, kuna mtu yeyote atakayejibu?!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ] “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu