Jumanne, 10 Rabi' al-thani 1448 | 2026/09/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Rabi' I 1448 Na: H 1448 / 042
M.  Ijumaa, 11 Septemba 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uislamu Pekee ndio Unaoweza Kuwaunganisha Waislamu na Kuufurusha Ukoloni, ambao Umeiacha Libya ikiburuta Mkia Wake kwa Masikitiko  
(Imetafsiriwa)

Inasikitisha sana kwamba Libya—nchi ya ukombozi wa awali na upinzani dhidi ya wavamizi, chimbuko la wanazuoni mashuhuri na mstari wa mbele katika kuhifadhi Qur’an Tukufu, nchi ya Omar Al-Mukhtar na wahifadhi wa Qur’an milioni moja—iwe uwanja wa mzozo kati ya dola za kikoloni, huku kichocheo chake kikiwa ni vijana wa Kiislamu, mali zao, na ardhi zao. Tangu dhalimu Muammar Gaddafi alipoondolewa madarakani mwishoni mwa mwaka 2011 hadi leo, wale wanaowania madaraka wameendelea kuitumbukiza nchi katika machafuko, huku wakitumikia maslahi ya dola za kikoloni.

Wanaowania madaraka wanaendelea kuigawa nchi katika maeneo ya Mashariki na Magharibi, kukiwa na serikali mbili; moja ikiongozwa na Abdul Hamid Dbeibah na yenye makao yake Tripoli, na nyingine ikiongozwa na Osama Hamad na yenye makao yake Benghazi; pamoja na majeshi mawili; moja likiwa Magharibi na kushirikiana na kile kinachoitwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Abdul Hamid Dbeibah, na jengine likiwa Mashariki mwa nchi likiongozwa na mrithi wa Haftar.

Katika hali nzuri zaidi, wanazungumzia mikutano ya kufikia makubaliano kuhusu namna ya kugawanya madaraka na umoja, kana kwamba suala la umoja wa Waislamu ni jambo la ikhtilafu na si jambo lililowekwa wazi na kuthibitishwa katika dini yetu tukufu!

Wakuu wa majeshi ya anga, majini, na ulinzi wa anga wanaoshirikiana na Serikali ya Umoja wa Kitaifa magharibi mwa Libya na vikosi vya mashariki mwa Libya walikubaliana kuhusu mpango wa kazi wa pamoja na mikakati ya utekelezaji ili kuimarisha ushirikiano na muungano katika nyanja mbalimbali za kijeshi, badala ya kuzungumzia umoja wa nchi na kumaliza hali ya mzozo wa kugombania madaraka! Na ili kudhihirisha upuuzi wa jitihada hizo na kukosekana kwa matumaini kwamba jitihada na mazungumzo hayo yataleta manufaa kwa nchi, taasisi ya kijeshi inaendesha mazungumzo hayo chini ya udhamini wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa na ndani ya mfumo wa kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini Geneva mnamo Oktoba 2020 kati ya pande zinazohusika katika mzozo wa Libya.

Hakika, suala la wajibu wa umoja wa Waislamu ni jambo lililowekwa wazi na Sharia, kutokana na kauli Yake (swt): [وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعاً وَلاَ تَفَرَّقُواْ] “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Aal-i-Imran:103]. Na kutokana na kauli yake (saw): «مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ فَاقْتُلُوهُ» “Yeyote atakayewajia wakati mambo yenu yameungana chini ya mtu mmoja, akitaka kuvunja umoja wenu au kugawanya jamii yenu, basi muuweni.” Na kauli yake (saw): «إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ فَاقْتُلُوا الْآخَرَ مِنْهُمَا» “Pindi kiapo cha utiifu kitakapotolewa kwa Makhalifa wawili, basi muuweni yule wa pili kati yao.”

Mnufaika pekee wa kutoelewana, mgawanyiko, na mapigano ya Waislamu ni mkoloni ambaye anataka nchi ibaki ikiwa imegawanyika na kutawanyika mikononi mwa vibaraka wake ili aweze kuendelea kupora utajiri wa nchi hiyo. Kwani mzozo kati ya vibaraka wa Uingereza na vibaraka wa Marekani ndio unaoiweka nchi katika mzunguko wa mgawanyiko na umwagaji damu, na ni mzozo ambao waliohasirika pekee ni Waislamu; kwa hivyo, watu wenye ikhlasi wa Libya—wenye mamlaka na maamuzi miongoni mwa makabila, na wanazuoni wema—lazima wawakamate mkono viongozi wa mzozo huo na pande zinazohusika ili kuiokoa nchi kutoka kwenye makucha ya ukoloni, na kuiunganisha chini ya bendera (Rayah) ya La ilaha illa Allah, Muhammad Rasul Allah, na sio bendera ya ukoloni.

Kwani Uislamu, ambao uliweza kuwaunganisha Al-Aws na Al-Khazraj, una uwezo wa kuwaunganisha watu wa Mashariki na Magharibi nchini Libya, na hakika, Waislamu wote duniani.

Anasema Mwenyezi Mungu (swt): [وَاذْكُرُواْ نِعْمَتَ اللّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاء فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَاناً وَكُنتُمْ عَلَىَ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ] “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” [Aal-i-Imran:103].

Basi njooni tuifanye Libya kuwa ni nukta ya nusra kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kwani katika hayo imo kheri ya dunia hii na Akhera.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.muslimworld.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) muslimworld.today

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu