Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 506
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
Kalima iliyoelekezwa kwa jamii ya Waislamu ili kuregesha uaminifu wake kwa Uislamu na kujiepusha na wafisadi, kwa kuzingatia hotuba ya mhalifu Netanyahu mbele ya bunge la Congress.
Khilafah itakomesha sera ya ubinafsishaji iliyowekwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, IMF, ambayo imesababisha uharibifu wa sekta ya nishati, mafuta na gesi, na badala yake itatabikisha hukmu ya umilikaji wa umma katika Uislamu, kuhusiana na nishati na madini.
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni taasisi ya kikoloni ikitoka kwa mkataba wa bretton woods, inatumika kuanzisha ukiritimba wa dola ya marekani katika biashara ya kimataifa.
Kwa kutenga asilimia 52 ya bajeti yote kwa malipo ya riba pekee, maslahi ya wananchi, serikali na usalama yako hatarini.
Mnamo tarehe 12 Juni 2024, Waziri wa Fedha wa Pakistan aliwasilisha bajeti ya serikali ya shirikisho kwa mwaka wa 2024-2025, ambayo ilisheheni ushuru mkubwa, na kusababisha hofu miongoni mwa watu. Bajeti hiyo ilipitishwa na bunge mnamo tarehe 28 Juni, baada ya kutoza ushuru zaidi, ambao haukuwa sehemu ya bajeti ya awali!
Ushiriki wa Hizb ut Tahrir/Kenya katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Ushiriki wa Hizb ut Tahrir/Ukraine katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Bajeti ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa imezua Balaa kwa Waislamu! Hukmu za Uislamu ndizo pekee zilizo na uwezo wa kuhafifisha migogoro mikubwa ya kiuchumi.