Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo 456
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Baada ya miezi kumi ya mauaji ya kila siku dhidi ya watu wa Gaza, ambayo yanatangazwa muda baada ya muda kwa sauti na picha za hali ya juu, kwa idadi, takwimu, ushuhuda na hukumu za mahakama... baada ya yote hayo, Bunge la Congress lilimpokea kiongozi wa Baraza la Vita huko Gaza, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Netanyahu, kwa karamu ya nderemo na shangwe kana kwamba yeye ni mmoja wa mashujaa wa watu wao. Sauti yao ya ndani ikisema: Tunataka kukupa ujira, Netanyahu, kwa kuwaua Waislamu wa Gaza kwa niaba yetu.
Huku Wamagharibi wakikata tamaa ya uwezo wa tawala vibaraka katika nchi za Kiislamu kuendelea kudhibiti na kutawala mambo, na uhakika wake kwamba Ummah unakaribia kuzifagilia mbali tawala hizi na kuziondoa, na hivyo kuondoa uwepo wao katika nchi zetu; kwa kuzingatia haya yote, hatua hii ilitoka kwa NATO, ili wao wenyewe waweze kusimamia utekelezaji wa mipango yao na kulinda maslahi yao katika ardhi zetu, na kulinda umbile la Kiyahudi.
Ndege za umbile halifu la Kiyahudi zilianzisha msururu wa mashambulizi ya kichokozi dhidi ya Yemen. Wakati wa mkutano wake jana, Baraza la Mawaziri la umbile hilo linalohusika na masuala ya usalama liliidhinisha shambulizi hilo dhidi ya Yemen, kwani uvamizi huo ulilenga vituo vya kuhifadhi mafuta na kituo cha umeme katika bandari ya Hodeidah.
Katika shambulizi la kiuhaini na lisilo na aibu, umbile halifu la Kiyahudi lilimuua mkuu wa afisi ya kisiasa ya Hamas jijiniTehran, ambapo Ndugu Ismail Haniyeh aliuawa shahidi alfajiri ya leo na adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Umma. Tunamuomba Mwenyezi Mungu rehema na msamaha wake na amjaalie miongoni mwa mashahidi. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutaregea.
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa, baada ya swala ya Ijumaa, visimamo katika mji wa Ankara Na mji wa Van chini ya kichwa. “Khiyana ya Watawala Yaiuwa Gaza!”
Mnamo asubuhi ya tarehe 31 Julai 2024, umbile la Kiyahudi lilimuua shahidi kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh katika shambulizi la kombora jijini Tehran, mji mkuu wa Iran. Siku moja kabla, umbile hilo la Kiyahudi lilimuua shahidi kamanda wa Hezbollah kwa kushambulia jengo la makaazi jijini Beirut, Lebanon. Hapo awali, umbile la Kiyahudi lilishambulia vituo mbalimbali katika bandari ya Hodeida nchini Yemen kwa ndege za kivita. Hii ni huku Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ikiwa imegeuzwa kuwa magofu katika kipindi cha miezi kumi iliyopita.
Sudan Tribune iliripoti jana, Jumamosi, Julai 27, 2024, ikinukuu taarifa iliyotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari wa Sudan, iliyosema: “Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari ilisema katika taarifa iliyopokelewa na Sudan Tribune kwamba watu waliokimbia makaazi yao mjini Kassala wanaishi kwenye mahema yaliyochakaa na kuzungukwa na maji kila upande, na watoto wao wanalia kwa njaa. Iliongeza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi, kwani watoto wawili walikufa kwa shoti ya umeme, na kuna vifo kutokana na kuumwa na nyoka na kesi zingine zisizojulikana.”
Mnamo siku ya Ijumaa, Agosti 2, 2024, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa maandamano katika mji wa Al-Qadarif baada swala ya Juma’a karibu na Jami’ Al-Atiq (Msikiti Mkongwe) katika Soko la Al-Qadarif. Maandamano hayo yalitaka kukomeshwa kwa vita na umwagaji damu ya Waislamu.