Afisi Kuu ya Habari: Ulinganizi wa Kiulimwengu Sehemu ya 61 – Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ulinganizi wa Kiulimwengu Sehemu ya 61 – Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume
Ulinganizi wa Kiulimwengu Sehemu ya 61 – Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume
Washiriki katika mjadala wa jopo, ulioandaliwa na Wizara ya Sheria na Chama cha Biashara na Viwanda katika mji mkuu, Sana'a, juu ya rasimu ya sheria ya kuzuia miamala ya riba iliyoandaliwa na Wizara ya Sheria, walipendekeza rasimu hiyo ipelekwe kwenye kamati ya kisheria, kiuchumi na Sharia kwa ajili ya uchunguzi kwa kuzingatia uzoefu wa Kiarabu na kimataifa.
Maadhimisho ya miaka kumi na mbili ya kuzinduliwa kwa mapinduzi ya Umma yanatuangukia tarehe 17 Disemba hii. Makafiri wa kikoloni wa Magharibi na vibaraka wao walio madarakani wanafanya kazi kwa njia na mbinu zote kuvunja utashi wa watu, kukandamiza ari yao ya kimapinduzi, na kuondoa jaribio lolote la kuleta mabadiliko makubwa kwa msingi wa Uislamu, hasa pale Uislamu na Khilafah ilipokuwa ndio rai jumla katika nchi za Kiislamu, ikiwemo Tunisia.
Ratiba ya mikutano ya kazi ya kuamua Kima cha chini cha Mshahara imekuwa wazi. Tume ya Uamuzi wa Kima cha Chini cha Mshahara, inayojumuisha mwajiriwa, mwajiri na wawakilishi wa serikali, itafanya mkutano wake wa kwanza mnamo Disemba 7 na mkutano wa pili mnamo Disemba 14 ili kuamua kima cha chini cha mshahara cha mwaka 2023.
Taharuki umezuka tena huko Kosovo kaskazini huku mamia ya Waserbia wakiweka vizuizi vya barabarani kwa kutumia mashini nzito katika vivuko viwili vya mpaka na Serbia, na kuzuia magari. Haya yanajiri kutokana na mvutano wa hivi majuzi wakati Kosovo ilipoamuru madereva kusalimisha nambari zao za leseni zilizotolewa na Serbia na badala yake kuweka nambari za Kosovo.
Wakati wa siku hizi, mnamo 1971, Pakistan iligawanywa katika sehemu mbili, ya kwanza iliitwa Pakistan, na nyingine, Bangladesh, baada ya kuwa wameunganishwa kama umbile moja kwa karne nyingi.
Mnamo Jumapili, Novemba 27, 2022, serikali ya Maeen Abdul Malik ilitia saini makubaliano na Mfuko wa Fedha wa Kiarabu (AMF) kusaidia mpango wa mageuzi ya kiuchumi, kifedha na kisarafu kwa kiasi cha dolari bilioni moja, kulingana na Shirika la Habari la Yemen.
Siku chache zilizopita, tuliona makundi, vyama, na taasisi zinazofungamana na Umoja wa Mataifa zikifanya kampeni zenye vichwa vinavyobeba maana zinazokinzana na herufi za kimsingi za Waislamu kwa upande mmoja, na hazina uhalisia wowote miongoni mwetu kwa upande mwingine.
Mnamo tarehe 30 Novemba, takriban watu 17 waliuawa na wengine 26 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika madrasa huko Aybak, mji mkuu wa mkoa wa Samangan kaskazini mwa Afghanistan. Wengi wa waliouawa wanaaminika kuwa watoto wenye umri wa miaka 9-15. Katika kipindi cha miezi 15 iliyopita, kumekuwa na mashambulizi kadhaa dhidi ya madrasa, ikiwemo mikoa ya Mazar-e-Sharif, Balkh na Kunduz.