Jumatatu, 29 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Dola za Kigaidi au wale Wanaoitwa Wanachama wa SCO Wazungumza kuhusu 'Vita dhidi ya Ugaidi' nchini Afghanistan!

Mnamo siku ya Ijumaa, Oktoba 14, 2022, New Delhi iliandaa mkutano wa baraza la Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) chini ya kichwa cha Muundo wa Kikanda wa Kupambana na Ugaidi (RAT). Baada ya mkutano huu, baadhi ya nchi wanachama ziliapa kutekeleza hatua za pamoja ili kukabiliana na vitisho vinavyotokana na makundi ya kimataifa ya kigaidi yanayoendesha operesheni zao kutoka Afghanistan.

Soma zaidi...

Kwa kukosekana Khilafah, Watoto wa Ummah wetu nchini Iraq Wanaanikwa kwa Hofu za Utaifa

Mnamo tarehe 29 Septemba 2022, shirika la Habari la ‘Arab News’ liliripoti juu ya mashambulizi ya droni yaliyoanzishwa na Iran kwa kile kinachoitwa mawakala wa waasi wa Kikurdi katika eneo hilo. Milipuko ilitokea katika mji wa Irbil, Kurdistan ya Iraq na kushambulia shule moja iliyokuwa imejaa wanafunzi. Waandishi wa habari katika eneo la tukio walisambaza picha za watoto wa shule waliotapakaa damu katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq.

Soma zaidi...

Watoto wa Afghanistan na Unafiki wa Kimagharibi

Tangu utawala wa Marekani uondoke Afghanistan na serikali ya Taliban kuchukua madaraka, maamuzi ya nchi za Magharibi yalianza kuongezeka, hasa baada ya kundi la Taliban kuchukua maamuzi ambayo Magharibi inayaona kuwa hayaendani na hadhara na mtindo wake wa maisha, kama vile kulazimisha niqab kwa wanawake na kutenganisha madarasa kati ya wanaume na wanawake, pamoja na maamuzi mengine.

Soma zaidi...

Je, Maandamano ya Iran Yanaweza Kufanikiwa?

Maandamano nchini Iran sasa yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja nchini Iran tangu kifo cha Mahsa Amini mikononi mwa polisi wa maadili wa Iran, alipokamatwa kwa kukiuka kanuni za mavazi za nchi hiyo. Maandamano hayo yaliyotokea ni makubwa zaidi utawala huo wa watu wa dini kuwahi kukabiliana nayo kwa muda mrefu.

Soma zaidi...

Uhakiki wa Habari 15/10/2022

Kushindwa vibaya kwa Urusi katika vita vya Ukraine chini ya uongozi wa Rais Vladimir Putin kunafichua kwa haraka udhaifu wa kweli wa dola ya Urusi. Wakati fulani karibu kuchukuliwa kuwa dola kuu yenye nguvu sawa na Marekani, sasa haijulikani ikiwa Urusi itaweza hata kuendelea kuhesabiwa miongoni mwa dola kubwa duniani.

Soma zaidi...

Usaliti na Ufisadi wa Mamlaka ya Palestina ni Jinai Kubwa Dhidi ya Palestina na Watu wa Palestina!

Abbas bwege na genge lake, ambao wamemsaliti Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake, tangu kutiwa saini kwa Mkataba wa khiyana wa Oslo, na wamekuwa wakifanya kazi kwa utaratibu na uratibu pamoja na umbile la Kiyahudi, ili kuimaliza ari ya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) miongoni mwa watu wa Palestina ili kukomesha “mateso ya Mayahudi,” wanashirikiana dori kwa njia ovu.

Soma zaidi...

Waislamu wa Pakistan Wapinga Vikali Usalimishaji wa Kashmir kwa Dola ya Kibaniani. Uongozi wowote Mpya wa Kijeshi Lazima Utangaze Jihad kwa ajili ya Ukombozi wa Kashmir, Kuthibitisha Utiifu wake kwa Uislamu na Waislamu

Mkuu wa Wanajeshi ya Pakistan (COAS) Jenerali Qamar Javed Bajwa mnamo tarehe 8 Oktoba 2022, Jumamosi, alihutubia gwaride la kufuzu kwa Kozi ndefu ya 146 katika Chuo cha Kijeshi cha Pakistan. Hotuba hiyo hakika haikumstahiki mkuu wa jeshi ambalo ni la sita kwa ukubwa zaidi duniani, linalochukuliwa kuwa la tisa kwa nguvu zaidi, linalomiliki makombora ya nyuklia na balestiki.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu