Ametokea kwa Mlango, Anaingia kwa Dirisha
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa mara nyengine tena, Amerika inafichua kiburi chake mbele ya ulimwengu. Onyo la Donald Trump kwamba “mambo mabaya yatatokea” isipokuwa Afghanistan ikabidhi Kambi ya Anga ya Bagram inaakisi sauti ile ile ya kibeberu ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifafanua sera ya Marekani kwa ardhi za Waislamu. Maneno kama haya sio lugha ya dola huru zinazoamiliana kwa usawa, bali ni maagizo ya mkoloni ambaye anaziona ardhi za Waislamu kama kituo cha kijeshi kwa ajili ya matamanio yake. Hii ndiyo hali halisi ya siasa za Magharibi: ushurutishaji, vitisho, na kudharau ubwana wa nchi zetu.



