Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 373
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa dolari bilioni 1.5 zimekusanywa kushughulikia hali ya watu wa Afghanistan.
Jumamosi, tarehe 8/1/2022, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ukiongozwa na Sheikh Nassir Ridha Muhammad Othman, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, akifuatana na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, na Ust. Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano,
Imetajwa katika kitabu cha “Shakhsiya ya Kiislamu” Juzuu ya Kwanza, katika mlango: “Haja ya Umma leo kwa wafasiri” tulipozungumzia kuhusu Waarabu kuacha kutumia baadhi ya matamshi kwa kutosheka na visawe ama matamshi yanayokaribiana nayo, maadamu maana yaliyokusudiwa yamenyooka.
Mnamo tarehe 9 Januari 2022, Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa, wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi huko Colombo, aliomba kupunguzwa kwa ulipaji wa deni kwa China.
Mamlaka za serikali ya Hasina hivi majuzi zimebomoa zaidi ya maduka 3000 ya Waislamu wa Rohingya katika kambi ya wakimbizi ya Kutupalong wilayani Cox's Bazar, na kuwaacha wakimbizi hao wasio na uwezo bila vyanzo vya mapato na mahitaji ya kila siku.
Mnamo 2021, katiba mpya ilipitishwa nchini Kyrgyzstan. Tangu wakati huo, juhudi zimefanywa kuoanisha sheria na katiba mpya.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, alizindua mpango ambao alisema ni wa kukusanya vyama vya Sudan ili kujiondoa katika mzozo wa sasa wa kisiasa kwa mashauriano na kile alichokiita washirika wa Sudan na wa kimataifa.
Hivi karibuni Bunge la Amerika limeidhinisha bajeti ya ulinzi ya dolari bilioni 777.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kutoka mwaka jana.
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa kongamano la kiuchumi katika Kituo cha Utamaduni cha Kocatape jijini Ankara lenye kichwa "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi katika Nukta Kumi!"