Jumamosi, 30 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Musiiangushe Gaza, Enyi Waislamu

Ni masikitiko kwa usaliti! Maumivu yake yanaumiza moyo. Hakika, usaliti ni mchungu zaidi kwa nafsi kuliko maumivu ya njaa, kifungo, na mateso. Wananchi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina wakiwemo watu wa Gaza wanautaka Umma wa Kiislamu kuwanusuru na kuwakomboa, kwa sababu udugu wa Kiislamu unawataka Waislamu kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwao.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Mwaliko wa Kuhudhuria Mkutano na Waandishi wa Habari

Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, tuna furaha kuwaalika ndugu zetu katika vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wenye hamu na mambo ya umma kuhudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari, ambapo msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan atatoa hotuba kwa anwani: "Wito kwa Watu wa Sudan: Ikamateni Darfur ili Isijiunge na Kusin"

Soma zaidi...

Kashmir Haiwezi Kukombolewa Bila Kubadilisha Uongozi Unaopoteza Fursa ya Dhahabu ya Kuikomboa Kashmir, kwa ajili ya Kumfurahisha Trump

Leo, tarehe 5 Agosti 2025, miaka sita imepita tangu kuunganishwa kwa lazima kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu na Raja Dahir wa zama hizi, Modi. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa nchini Marekani, kuisalimisha Kashmir ilikuwa ni usaliti wa wazi wa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan wa wakati huo, serikali ya Bajwa-Imran. Miezi michache tu baadaye, Jenerali Bajwa aliendeleza usaliti huu kwa kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano, na Dola ya Kibaniani kuhusiana na Kashmir. Hata hivyo, usaliti huu dhidi ya Waislamu wanaodhulumiwa na wanyonge wa Kashmir uliendelea hata zaidi ya hapo.

Soma zaidi...

Njia ya Kujiondolea Dhambi ya Kuwatelekeza Waislamu wa Palestina, ni Kujitahidi Mchana na Usiku Kusimamisha Khilafah Rashida, na Kukusanya Majeshi

Kwa vile majeshi ya Waislamu hayakusonga kuinusuru Gaza, baba mwengine aliyedhulumiwa, Abu Umar, aliuawa shahidi, alipokuwa akiwatafutia watoto wake chakula. Alipokuwa akingoja kupokea msaada, risasi ya mdunguaji Myahudi muoga ilipenya kichwa chake. Yule rafiki aliyeuleta mwili wake alikuwa na njaa kwa siku tano, na akarudi kutoka kwenye kizingiti cha mlango wa shahada, labda kuuawa shahidi hivi karibuni. Hili sio tukio moja pekee. Makumi ya matukio kama haya yanashuhudiwa moja kwa moja kila siku, na Umma wa bilioni mbili.

Soma zaidi...

“Siku ya Uhuru” ya 78 Pakistan Itakuwa Huru Kupitia Kuanzishwa kwa Khilafah Rashida

Chini ya mfumo wa sasa wa kimataifa, kile kinachoitwa uhuru si kitu zaidi ya usanii wa mchezo wa kuigiza, kwan maana ukombozi wa kweli (tahrir) uko pale tu dola inapoweza kupanga mambo yake ya ndani na mahusiano ya nje kwa mujibu wa itikadi yake. Watu wanaoamini “La ilaha illa Allah Muhammadur RasulAllah” kamwe hawatakombolewa kikweli mpaka watabikishe katika ardhi yao mfumo wa Kiislamu wa utawala, uchumi, jamii, elimu, na mahakama, pamoja na sera ya kigeni yenye msingi wa Da‘wah na Jihad. Hii ndiyo maana halisi ya uhuru, na katika suala hili, Pakistan bado haijakombolewa!

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan: “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.”

Hii ni hotuba kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Waislamu kuhusiana na faradhi ya Shariah ya kuwanusuru Waislamu walio chini ya mamlaka ya dola za kikafiri na makafiri ambao hawajahamia kwenye Nyumba ya Uislamu (Dar ul Islam), iwe kwa kuwazuia utekelezaji wa ibada zao za kidini au kwa kuwadhulumu.

Soma zaidi...

Ndoto ya Kikoloni ya ‘Dola Mbili’ kwa Palestina

Wakati Gaza ikiendelea kuungua, huku makumi ya watu wakiuawa katika Ukanda huo kila siku, huku wakaazi wake wakiendelea kufa kwa njaa, na wakati ghasia zikiongezeka katika Ukingo wa Magharibi mikononi mwa uvamizi wa kinyama wa Kizayuni, kumekuwa na msukumo mpya, hasa wa baadhi ya nchi za Magharibi, kwa ajili ya ‘Suluhisho la Dola Mbili’ kwa Palestina ambayo wanatoa hoja kuwa litaweza kutatua mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo. Ufaransa, Uingereza na Canada miongoni mwa mataifa mengine zimetangaza nia yao ya kuitambua dola ya Palestina, ikiwa masharti maalum yatatimizwa.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu