Jumamosi, 05 Muharram 1448 | 2026/06/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mjadala juu ya Upandaji wa Malori ya Kuhitimu Unafichua Chuki iliyokithiri ya Vyombo vya Habari na Wanasiasa wa Denmark dhidi ya Uislamu

Wiki hii iliyopita kumeshuhudiwa vurumai kubwa la vyombo vya habari na kisiasa kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii ambapo Waislamu waliwapongeza wahitimu wa mwaka huu huku pia wakiwasilisha mtazamo wa Kiislamu kuhusu kupanda malori ya kuhitimu yenye sifa ya ulevi na tabia mbaya.

Soma zaidi...

Utambuzi wa Urusi wa Serikali ya Afghanistan: Hatua Zaidi ya Kuzuia Kuibuka kwa Mfumo wa Kiislamu katika Kanda hii

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inauona utambuzi huu kama sehemu ya mchakato mpana ambao kwao utawala wa sasa utayeyushwa hatua kwa hatua ndani ya mfumo wa kimataifa wa kisekula wa dola ya kitaifa. Mfumo huu, baada ya muda, utaiweka mbali serikali hii na lengo kuu la Kiislamu la kusimamisha na kubeba Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, utambuzi huo unaweza kuigeuza Afghanistan kuwa uwanja wa vita vya kiushindani kati ya dola za kikanda na kimataifa.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh Iliandaa Maandamano na Matembezi ya kupinga Uhamishaji wa India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa Mtutu wa Bunduki

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, iliandaa maandamano na matembezi leo (Ijumaa, 4 Julai 2025) baada ya swala ya Ijumaa katika misikiti mbalimbali ya Dhaka na Chittagong kupinga uhamishaji unaoendelea wa India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa mtutu wa bunduki. Wanachama mbalimbali wa Hizb ut Tahrir walitoa hotuba katika maandamano hayo ambayo yalimalizika sambamba na matembezi.

Soma zaidi...

Uhamishaji wa Dola ya Hindutva ya India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa Mtutu wa Bunduki ni Uadui wa Wazi kwa Waislamu kama ule wa Umbile Haramu la Kiyahudi

Serikali ya Hindutva ya Modi inaendelea kuongeza kiwango cha ukandamizaji na mateso, ikiwa ni pamoja na kubomoa nyumba za Waislamu wa India na kuwapeleka uhamisho kwa nguvu usio wa haki. Kupitia hili kimsingi wanafuata nyayo za dola haramu ya Kiyahudi ‘Israel’. Hivi karibuni, hata wanawatendea Waislamu wa India kama wanyama kwa kuwaita wahamiaji haramu na kuwarudisha mamia yao nchini Bangladesh kwa mtutu wa bunduki, wakipuuza kile kinachoitwa michakato yao ya kisheria ya kitaifa na kimataifa. "Walitutendea kama wanyama," alisema mwanamke mmoja anayeitwa Rahima Khatun. "Tulipinga kwamba sisi ni Wahindi, kwa nini tuingie Bangladesh? Lakini walituelekezea bunduki na kutishia, 'Ikiwa hamtakwenda kwa huko, tutakupigeni risasi.' Baada ya kusikia milio minne ya risasi kutoka upande wa India, tuliogopa sana na haraka tukavuka mpaka kwa miguu". [Ripoti ya FP].

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria na Kushiriki katika Kikao cha Masuala ya Ummah

Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tunafuraha kuwaalika wanataaluma wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wanaohusika na masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika Kikao cha Masuala ya Ummah wa kila mwezi, ambacho mwezi huu kitakuwa na kichwa: “Hatari ya Kuyatazama Mamlaka Kama Keki Inayopaswa Kugawanywa”

Soma zaidi...

Haya ndiyo Matendo ya Umoja wa Mataifa... Mutaendelea Kuwahadaa Wananchi Mpaka Lini? Ni Kipi Kipya? Yako wapi Mabadiliko, Ee Wizara ya Ujenzi na Mabadiliko?

Mnamo Jumapili, tarehe 29/6/2025, jijini Sana'a, Waziri wa Masuala ya Kijamii na Leba, Samir Baja'ala, alifanya mkutano na kamati za maandalizi ya Kongamano la Vyama vya Ushirika la 2025, litakaofanyika mapema Julai 2025. Mkutano huo ulihudhuriwa na Ali Al-Razami, Katibu Mdogo wa Wizara ya Sekta ya Maendeleo na Nasser Al-Kahili, Mkurugenzi wa Afisi ya Masuala ya Kijamii na Afisi ya Leba katika Sekretarieti Kuu.

Soma zaidi...

Trump na Netanyahu Wanajigamba na Kujisifu Huku Watawala Wetu Wakikaa Kimya Mithili ya Wafu Makaburini Mwao!

Vita kati ya Iran na umbile la Kiyahudi vimemalizika, na jinai za Mayahudi mjini Gaza hazikukoma wakati wa vita hivyo, wala hadi wakati huu. Marekani ilifanya ujanja wa kiusanii, ikidai kuwa imeangamiza uwezo wa nyuklia wa Iran. Hatua hii imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kukutana na wale wanaojiita mawaziri wa Troika wa Ulaya, ambao walikuwa sehemu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran kabla ya Marekani kujitoa katika mazungumzo hayo wakati wa muhula wa kwanza wa Trump. Iran pia ilifanya mbwembwe za kiusanii kwa kurusha makombora kadhaa katika Kambi ya Kimarekani ya Al Udeid nchini Qatar, baada ya kuifahamisha Marekani kuhusu hilo, kama Trump mwenyewe alivyosema.

Soma zaidi...

Harakati ya Taliban na Fursa ya Kusimamisha Khilafah

Maisha haya ya dunia ni kama dimbwi la hasara, ambalo ni wale tu wanaojua kukamata fursa ndio wataokolewa. Kwa sababu hii, Siku ya Kiyama inaitwa “Siku ya Majuto,” kwa sababu watu wengi wamezama katika hasara ya kidunia, na wameshindwa kutumia fursa za thamani walizopewa katika maisha yao. Walipoteza kwa urahisi nyakati za dhahabu alizozitoa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya mwamko na izza ya Umma.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu