Ijumaa, 17 Ramadan 1447 | 2026/03/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Jibu la Swali: Mashambulizi ya Droni na Yanayojiri katika Vita nchini Sudan

Siku za hivi karibuni zimeshuhudia maendeleo ya ajabu katika vita. Droni zilishambulia Port Sudan, mji mkuu wa utawala, kwa siku sita mfululizo, na kushambulia uwanja wa ndege wa kiraia, kambi ya anga, na maghala ya mafuta, na kusababisha mgogoro wa mafuta kote nchini. Droni pia zilishambulia mji wa Kassala kwenye mpaka wa Eritrea upande wa mashariki, pamoja na miji mingine. Haya yote yalisababisha vikosi vya jeshi kuondoka kuelekea upande wa El Fasher na kuzingatia kulinda Sudan mashariki, kama BBC ilivyoripoti mnamo tarehe 10/5/2025. Je, hii ina maana kwamba shambulizi la mashariki mwa Sudan linalenga kuliondoa jeshi kutoka Darfur, na kuiacha ikiwa chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) pekee? Je, matukio haya ni utangulizi wa Jukwaa la Jeddah (kongamano la mazungumzo)? Au kuna malengo mengine?

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Uholanzi: Semina Jijini Amsterdam “Gaza Yalilia Msaada!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa, na kupoteza zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 180,000 hadi sasa, Hizb ut Tahrir, Uholanzi iliandaa semina katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam yenye kichwa: “Gaza Yalilia Msaada!”

Soma zaidi...

Hatimaye, Dhalimu Trump Anahitimisha Ziara yake katika Kanda hii

Trump alianza ziara yake nchini Saudi Arabia mnamo Mei 13, 2025, ikifuatiwa na Qatar mnamo Mei 14, 2025, akihitimisha safari yake nchini Imarati mnamo Mei 15, 2025, na kuhitimisha ziara yake mnamo Mei 16, 2025. Kisha aliandamanisha ziara hii kwa udanganyifu wake kwamba hatazuru umbile la Kiyahudi, kuwakejeli wajinga wanaodai kuwa uungaji mkono wa Trump kwa umbile la Kiyahudi umetikiswa! Hii ni licha ya ukweli kwamba umbile la Kiyahudi lilipanua mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza baada ya Trump kuondoka katika nchi hizo tatu.

Soma zaidi...

Kukabidhi Uendeshaji wa Operesheni za "Bohari la Kontena la New Mooring " kwa Kampuni ya Wakoloni yenye Ushawishi wa Marekani "DP World" kutatishia Ubwana wa Nchi

Bila kujali ubwana wa nchi, serikali ya mpito inaendelea na mchakato wa kukabidhi huduma na mabohari mbalimbali ya Bandari ya Chittagong muhimu kimkakati na kiuchumi kwa wageni kwa jina la kuongeza uwezo wa bandari kwa kisingizio cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI). Kama sehemu ya hili, mchakato wa kukabidhi Bohari Kuu la Kontena la New Mooring (NCT) la Bandari ya Chittagong linalojitosheleza na la juu zaidi la kuzalisha mapato kwa kampuni ya DP World uko katika hatua zake za mwisho (Daily Jugantor, Mei 6, 2025).

Soma zaidi...

Mamlaka ya Palestina ilimuua Rami Zahran, Kisha Mzee Mmoja, Ikikamilisha Uhalifu wake Dhidi ya Watu wa Palestina

Mnamo siku ya Jumanne,13/5/2025, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Palestina vilimuua kijana Rami Zahran kutoka kambi ya wakimbizi ya Al-Far'a huko Tubas. Kisha wakafuatilisha hili kwa kumuua mzee mmoja (Abu Khalil al-Saba'neh) kutoka mji wa Jenin. Huu ni mwendelezo wa jinai zake dhidi ya watu wa Palestina, zikiwemo za mauaji, uchomaji moto, ukamataji, uvamizi wa misikiti, na unyang'anyaji mali ya Wapalestina kinyume cha sheria, kula mali zao kwa njia ya dhambi na fujo.

Soma zaidi...

Mwisho wa Enzi ya Awami League, Chama Kinara cha Siasa za Kisekula - ni Onyo la Kihistoria kwa Vyama Vilivyopo vya Kisiasa na Nyuso Mpya za Kisiasa

Kwa kuanguka kwa dhalimu Hasina na tangazo rasmi la kupigwa marufuku kwa shughuli zote za chama kiovu cha Awami League, enzi ya giza ya siasa za chama kikuu cha kisekula -Awami League imekamilika. Kuangamia huku kwa Awami League, mrithi wa 'All India Muslim League' iliyoanzishwa mwaka wa 1906, hakutokani na mlingano wa kisiasa wa mamlaka ya kundi lolote la kisiasa, bali ni ukweli wa kihistoria na usioepukika. Hamu ya Waislamu wa India ni kuishi chini ya utawala wa Kiislamu-Khilafah.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: India, Pakistan, na Usitishaji Mapigano

Trump alitangaza kwa mshangao jana, Jumamosi, katika chapisho kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Kijamii (Truth Social platform), kwamba "Baada ya usiku mrefu wa mazungumzo yaliyopatanishwa na Marekani, ninafurahi kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubali kusitishwa kwa mapigano kamili na mara moja, "na kuzisifu nchi zote mbili kwa kutumia busara na akili kubwa." (Al Jazeera, 11/5/2025) ... ni upi ukweli katika uhasama na mzozo huu? Je, Mkataba wa Maji wa Indus ni nini haswa ambao India imeusitisha kwa muda? Je, Marekani inahusika katika kuanzisha shambulizi hilo na pia kulisitisha?

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Ewe Mwenyezi Mungu! Jaaliya Ukombozi wa Kashmir uwe Utangulizi wa Ukombozi wa Palestina!

Mabadilishano ya makombora kati ya Pakistan na India yanaendelea katika njia nyingi za kusitisha mapigano huko Kashmir baada ya India kushambulia kwa mabomu maeneo tisa ndani ya Pakistan usiku wa Mei 6, ambayo ilisema ni "miundombinu ya kigaidi iliyohusika na shambulizi la silaha huko Kashmir" mwezi uliopita. Suluhisho la kivitendo la kusonga mbele haliwezi kuwa mzozo mdogo, lakini lazima liwe ukombozi wa kina wa maeneo yanayokaliwa kimabavu.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu