Ummah Kati ya Uwepo Tu na Kazi Halisi, Kutokuwepo au Kutoweka? Sababu na Mbinu za Uchangamshaji
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni muhimu kutofautisha kati ya uwepo wa awali wa jambo na maelezo ya hali yake. Kwa mfano, uwepo wa kimwili wa gari ni wa kudumu, lakini kuharibika au kutotembea kwake kunaelezea hali yake. Vile vile, uwepo wa Ummah wa Kiislamu ni wa kweli na imara, wenye kumiliki vipengee vyake muhimu: Aqidah (itikadi) inayounganisha na mifumo ya maisha inayotokana na aqidah hiyo.



