Kuwakataa Wanariadha wa ‘Israel’: Kipimo Halisi cha Msimamo Madhubuti wa Indonesia?
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Indonesia: Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ilikataa rufaa ya Shirikisho la Michezo ya Viungo (Gymnastics) la ‘Israel’ (IGF) kuruhusu wanariadha wake kushiriki Mashindano ya Dunia ya Sanaa za Gymnastiki jijini Jakarta, Indonesia, kuanzia Oktoba 19–25, 2025. Serikali ya Indonesia iliwanyima viza wachezaji sita wa mazoezi ya viungo wa ‘Israel’, ikionyesha uungaji mkono kwa Wapalestina na shinikizo la ndani. IGF ilkata rufaa kwa CAS na Shirikisho la Kimataifa la Gymnastiki (FIG), ikiomba hatua za kuhakikisha ushiriki au kubatilisha michezo hiyo. CAS ilitupilia mbali rufaa zote mbili, na FIG ilisema haina mamlaka juu ya maamuzi ya visa. Indonesia ilithibitisha tena msimamo wake, ikiegemea katika sera yake ya kigeni na hisia za umma.



